2 Samuel 19:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shimei alikwenda pamoja na Wabenyamini 1,000. Siba mtumishi wa jamaa ya Shauli, pamoja na watoto wake kumi na watumishi ishirini, walikwenda haraka mtoni Yordani kumtangulia mfalme Daudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pamoja naye walikuwa Wabenyamini elfu moja wakiwa wamefuatana na Siba, msimamizi wa nyumba ya Sauli, pia wanawe kumi na watano, na watumishi ishirini. Wakaharakisha kwenda Yordani, mahali mfalme alipokuwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Watu elfu wa Benyamini walikuwa pamoja naye, na huyo Siba mtumwa, nyumba ya Sauli, na hao wanawe kumi na watano, na watumwa wake ishirini pamoja naye; wakavuka Yordani mbele ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shimei alikwenda pamoja na Wabenyamini 1,000. Siba mtumishi wa jamaa ya Shauli, pamoja na watoto wake kumi na watumishi ishirini, walikwenda haraka mtoni Yordani kumtangulia mfalme Daudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pamoja naye walikuwapo Wabenyamini elfu moja wakiwa wamefuatana na Siba, msimamizi wa nyumba ya Sauli, pia wanawe kumi na watano, na watumishi ishirini. Wakaharakisha kwenda Yordani, mahali mfalme alipokuwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pamoja naye walikuwepo Wabenyamini elfu moja wakiwa wamefuatana na Siba, msimamizi wa nyumba ya Sauli, pia wanawe kumi na watano, na watumishi ishirini. Wakaharakisha kwenda Yordani, mahali mfalme alipokuwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Watu elfu moja wa Benyamini walikuwa pamoja naye, na huyo Siba mtumishi wa nyumba ya Sauli, na hao wanawe kumi na watano, na watumishi wake ishirini pamoja naye; wakavuka Yordani mbele ya mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shimei alikwenda pamoja na Wabenyamini 1,000. Siba mtumishi wa jamaa ya Shauli, pamoja na watoto wake kumi na watumishi ishirini, walikwenda haraka mtoni Yordani kumtangulia mfalme Daudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pamoja naye wakaja watu elfu toka nchi ya Benyamini, hata Siba, mtumishi wa nyumbani mwa Sauli, akaja na wanawe 15 na watumishi wake 20. Wao walikuwa wamevuka Yordani, mfalme alipokuwa hajaja bado.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Watu elfu wa Benyamini walikuwa pamoja naye, na huyo Siba mtumwa, nyumba ya Sauli, na hao wanawe kumi na watano, na watumwa wake ishirini pamoja naye; wakavuka Yordani mbele ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simei mwana wa Gera, wa kabila la Benjamina, kutoka Bahurimu, alifanya haraka kwenda pamoja na watu wengine kwa kumupokea mufalme Daudi.