2 Samuel 19:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakavuka kwenye kivuko ili kuisindikiza jamaa ya mfalme na kumfanyia mfalme yote aliyoyapenda. Shimei mwana wa Gera akaja, akajitupa mbele ya mfalme, akasujudu, wakati mfalme alipokuwa karibu kuvuka mto Yordani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakavuka kivuko ili kuwachukua watu wa nyumbani mwa mfalme ili kuwavusha na kufanya kila kitu alichotaka. Shimei mwana wa Gera alipovuka Yordani, akaanguka kifudifudi mbele ya mfalme,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ikavuka mashua ili kuwavusha jamaa ya mfalme, na kufanya aliyoyaona kuwa mema. Ndipo Shimei, mwana wa Gera, akamwangukia mfalme alipokuwa amevuka Yordani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakavuka kwenye kivuko ili kuisindikiza jamaa ya mfalme na kumfanyia mfalme yote aliyoyapenda. Shimei mwana wa Gera akaja, akajitupa mbele ya mfalme, akasujudu, wakati mfalme alipokuwa karibu kuvuka mto Yordani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakavuka kivuko ili kuwachukua watu wa nyumbani mwa mfalme ili kuwavusha na kufanya kila kitu alichotaka. Shimei mwana wa Gera alipovuka Yordani, akaanguka kifudifudi mbele ya mfalme,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakavuka kivuko ili kuwachukua watu wa nyumbani mwa mfalme ili kuwavusha na kufanya kila kitu alichotaka. Shimei mwana wa Gera alipovuka Yordani, akaanguka kifudifudi mbele ya mfalme,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ikavuka mashua ili kuwavusha jamaa ya mfalme, na kufanya aliyoyaona kuwa mema. Ndipo Shimei, mwana wa Gera, akamwangukia mfalme alipokuwa amevuka Yordani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakavuka kwenye kivuko ili kuisindikiza jamaa ya mfalme na kumfanyia mfalme yote aliyoyapenda. Shimei mwana wa Gera akaja, akajitupa mbele ya mfalme, akasujudu, wakati mfalme alipokuwa karibu kuvuka mto Yordani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtumbwi wa kuwavusha walio wa nyumbani mwa mfalme ulipofika ng'ambo ya huko, mfalme aone, wanavyomfanyizia kazi nzuri, ndipo, Simei, mwana wa Gera, alipojiangusha chini machoni pa mfalme, alipotaka kuuvuka Yordani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ikavuka mashua ili kuwavusha jamaa ya mfalme, na kufanya aliyoyaona kuwa mema. Ndipo Shimei, mwana wa Gera, akamwangukia mfalme alipokuwa amevuka Yordani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simei alikwenda pamoja na watu wa kabila la Benjamina elfu moja. Siba mutumishi wa jamaa ya Saulo, pamoja na watoto wake kumi na watumishi makumi mbili, walikwenda haraka kwenye muto Yordani kumutangulia mufalme Daudi.