2 Samuel 19:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, mimi mtumishi wako ninajua kwamba nilitenda dhambi. Hii ndiyo sababu nimekuja leo, nikiwa wa kwanza katika kabila la Yosefu, kuja kukulaki wewe bwana wangu, mfalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana mimi mtumishi wako najua nimefanya dhambi, lakini leo nimekuja hapa kama wa kwanza wa nyumba yote ya Yusufu kushuka na kumlaki bwana wangu mfalme.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa mimi mtumwa wako najua ya kwamba nimekosa; kwa hiyo, tazama, nimekuja leo, wa kwanza wa nyumba yote ya Yusufu, kushuka ili nimlaki bwana wangu mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, mimi mtumishi wako ninajua kwamba nilitenda dhambi. Hii ndiyo sababu nimekuja leo, nikiwa wa kwanza katika kabila la Yosefu, kuja kukulaki wewe bwana wangu, mfalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana mimi mtumishi wako najua nimefanya dhambi, lakini leo nimekuja hapa kama wa kwanza wa nyumba yote ya Yosefu kushuka na kumlaki bwana wangu mfalme.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana mimi mtumishi wako najua nimefanya dhambi, lakini leo nimekuja hapa kama wa kwanza wa nyumba yote ya Yusufu kushuka na kumlaki bwana wangu mfalme.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa mimi mtumishi wako ninajua ya kwamba nimekosa; kwa hiyo, tazama, nimekuja leo, wa kwanza wa nyumba yote ya Yusufu, kushuka ili nimlaki bwana wangu mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, mimi mtumishi wako ninajua kwamba nilitenda dhambi. Hii ndiyo sababu nimekuja leo, nikiwa wa kwanza katika kabila la Yosefu, kuja kukulaki wewe bwana wangu, mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtumwa wako anajua, ya kuwa mimi nimekosa; kwa hiyo unaniona leo, ya kuwa mimi ni wa kwanza wa mlango wote wa Yosefu, aliyeshuka kumwendea bwana wangu mfalme njiani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa mimi mtumwa wako najua ya kwamba nimekosa; kwa hiyo, tazama, nimekuja leo, wa kwanza wa nyumba yote ya Yusufu, kushuka ili nimlaki bwana wangu mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simei akamwambia mufalme: “Ninakuomba, bwana wangu mufalme, usinihesabu kuwa na kosa wala kukumbuka kosa nililofanya siku ile ulipokuwa ukiondoka Yerusalema. Ninakuomba usiyaweke hayo ndani ya moyo.