2 Samuel 19:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, ikawa alipofika Yerusalemu kumlaki mfalme, Daudi alimwuliza, “Je, Mefiboshethi, kwa nini hukuandamana pamoja nami?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipotoka Yerusalemu kuja kumlaki mfalme, basi mfalme akamuuliza, “Mefiboshethi, kwa nini hukufuatana nami?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ikawa, alipofika Yerusalemu kumlaki mfalme, mfalme akamwambia, Mbona hukwenda pamoja nami, Mefiboshethi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, ikawa alipofika Yerusalemu kumlaki mfalme, Daudi alimwuliza, “Je, Mefiboshethi, kwa nini hukuandamana pamoja nami?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati alipotoka Yerusalemu kuja kumlaki mfalme, mfalme akamwuliza, “Mefiboshethi, kwa nini hukufuatana nami?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati alipotoka Yerusalemu kuja kumlaki mfalme, mfalme akamuuliza, “Mefiboshethi, kwa nini hukufuatana nami?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ikawa, alipofika Yerusalemu kumlaki mfalme, mfalme akamwambia, Mbona hukwenda pamoja nami, Mefiboshethi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, ikawa alipofika Yerusalemu kumlaki mfalme, Daudi alimwuliza, “Je, Mefiboshethi, kwa nini hukuandamana pamoja nami?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, alipotoka Yerusalemu kumwendea mfalme njiani, mfalme akamwuliza: Sababu gani hukuenda pamoja na mimi, Mefiboseti?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ikawa, alipofika Yerusalemu kumlaki mfalme, mfalme akamwambia, Mbona hukwenda pamoja nami, Mefiboshethi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mefiboseti mujukuu wa Saulo alikwenda vilevile kumupokea mufalme Daudi. Tangu siku ile mufalme alipoondoka Yerusalema mpaka wakati aliporudi salama, Mefiboseti alikuwa hajapata kunawa miguu yake, kukata ndevu zake wala hakujali kufua nguo zake.