2 Samuel 19:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, amenisingizia kwako, ee bwana wangu mfalme. Lakini wewe, bwana wangu mfalme, uko kama malaika wa Mungu. Fanya lolote unaloona ni jema kwako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye amemchongea mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme. Bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu, kwa hiyo fanya lolote linalokupendeza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye amenisingizia mimi mtumwa wako kwa bwana wangu mfalme; lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu; utende basi yaliyo mema machoni pako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, amenisingizia kwako, ee bwana wangu mfalme. Lakini wewe, bwana wangu mfalme, uko kama malaika wa Mungu. Fanya lolote unaloona ni jema kwako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye amemchongea mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme. Bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu, kwa hiyo fanya lo lote linalokupendeza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye amemchongea mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme. Bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu, kwa hiyo fanya lolote linalokupendeza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye amenisingizia mimi mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme; lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu; utende basi yaliyo mema machoni pako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, amenisingizia kwako, ee bwana wangu mfalme. Lakini wewe, bwana wangu mfalme, uko kama malaika wa Mungu. Fanya lolote unaloona ni jema kwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yule amemsingizia mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme, lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu, na ufanye yaliyo mema machoni pako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye amenisingizia mimi mtumwa wako kwa bwana wangu mfalme; lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu; utende basi yaliyo mema machoni pako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mefiboseti akasema: “Ee bwana wangu mufalme, mutumishi wangu alinidanganya. Maana, mimi mutumishi wako, nilimwambia: ‘Unitandikie punda nipate kupanda juu yake kwenda pamoja na mufalme’, maana mimi mutumishi wako ni kilema.