2 Samuel 19:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Barzilai alikuwa mzee sana, mwenye umri wa miaka themanini. Naye Barzilai alikuwa amemtunza mfalme alipokaa huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa tajiri sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Barzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amempatia mfalme mahitaji alipokuwa anaishi huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa mtu tajiri sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye huyo Barzilai alikuwa mzee sana, amepata umri wa miaka themanini; naye amemlisha mfalme hapo alipokuwapo Mahanaimu; kwa kuwa alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Barzilai alikuwa mzee sana, mwenye umri wa miaka themanini. Naye Barzilai alikuwa amemtunza mfalme alipokaa huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa tajiri sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Barzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amempatia mfalme mahitaji wakati alipokuwa anaishi huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa mtu tajiri sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Barzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amempatia mfalme mahitaji wakati alipokuwa anaishi huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa mtu tajiri sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye huyo Barzilai alikuwa mzee sana, alikuwa na umri wa miaka themanini; naye amemlisha mfalme hapo alipokuwapo Mahanaimu; kwa kuwa alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Barzilai alikuwa mzee sana, mwenye umri wa miaka themanini. Naye Barzilai alikuwa amemtunza mfalme alipokaa huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa tajiri sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Barzilai alikuwa mzee mwenye miaka 80, naye ndiye aliyemtunza mfalme, alipokaa Mahanaimu, kwani alikuwa mtu mkuu sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye huyo Barzilai alikuwa mzee sana, amepata umri wa miaka themanini; naye amemlisha mfalme hapo alipokuwapo Mahanaimu; kwa kuwa alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Barzilayi wa Gileadi alikuwa amefika kutoka Rogelimu. Alikuwa amekwenda pamoja na mufalme kwenye muto Yordani kwa kumusindikiza mpaka ngambo ya muto.