2 Samuel 19:38 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akamwambia, “Kimhamu atakwenda nami, na nitamtendea lolote lililo jema kwako. Na lolote utakalotaka nikutendee, nitakutendea.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akamwambia Barzilai, “Kimhamu atavuka Yordani pamoja nami, nami nitamtendea lolote litakalokupendeza. Nawe kitu chochote unachotaka kutoka kwangu nitakutendea.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akajibu, Haya, Kimhamu na avuke pamoja nami, nami nitamtendea yaliyo mema machoni pako wewe; na kila utakalotaka kwangu, mimi nitalifanya kwa ajili yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akamwambia, “Kimhamu atakwenda nami, na nitamtendea lolote lililo jema kwako. Na lolote utakalotaka nikutendee, nitakutendea.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akamwambia Barzilai, “Kimhamu atavuka Yordani pamoja nami, nami nitamtendea lo lote litakalokupendeza. Nawe kitu cho chote unachotaka kutoka kwangu nitakutendea.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akamwambia Barzilai, “Kimhamu atavuka Yordani pamoja nami, nami nitamtendea lolote litakalokupendeza. Nawe kitu chochote unachotaka kutoka kwangu nitakutendea.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akajibu, Haya, Kimhamu na avuke pamoja nami, nami nitamtendea yaliyo mema machoni pako wewe; na kila utakalotaka kwangu, mimi nitalifanya kwa ajili yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akamwambia, “Kimhamu atakwenda nami, na nitamtendea lolote lililo jema kwako. Na lolote utakalotaka nikutendee, nitakutendea.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akajibu: Basi, Kimuhamu atakwenda huko pamoja na mimi, nami nitamfanyizia yaliyo mema machoni pangu, nayo yote, utakayonitakia, nitakufanyizia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akajibu, Haya, Kimhamu na avuke pamoja nami, nami nitamtendea yaliyo mema machoni pako wewe; na kila utakalotaka kwangu, mimi nitalifanya kwa ajili yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninakuomba uniruhusu mimi mutumishi wako, nikufie katika muji wangu, karibu na kaburi la baba yangu na mama yangu. Lakini huyu mutumishi wako Kimuhamu, umuruhusu aende pamoja nawe bwana wangu mufalme, na umutendee yeye lolote unaloona ni zuri.”