2 Samuel 19:42 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Yuda wakawaambia watu wa Israeli, “Kwa sababu mfalme ni ndugu yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirika kuhusu jambo hili? Je, tumekula chochote wakati wowote kwa gharama ya mfalme? Au je, yeye ametupa zawadi yoyote?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanaume wote wa Yuda wakawajibu wanaume wa Israeli, “Tulifanya hivi kwa sababu mfalme ni jamaa yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirikia jambo hili? Je, tumekula kitu chochote cha mfalme? Je, tumejichukulia kitu chochote kwa ajili yetu wenyewe?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo watu wote wa Yuda wakawajibu hao watu wa Israeli, Ni kwa sababu mfalme ndiye wa jamaa yetu; mbona basi ninyi mmekasirika kwa ajili ya jambo hili? Je! Sisi tumekula kitu cha mfalme? Ama ametupa sisi zawadi yo yote?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Yuda wakawaambia watu wa Israeli, “Kwa sababu mfalme ni ndugu yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirika kuhusu jambo hili? Je, tumekula chochote wakati wowote kwa gharama ya mfalme? Au je, yeye ametupa zawadi yoyote?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wote wa Yuda wakawajibu watu wa Israeli, “Tulifanya hivi kwa sababu mfalme ni jamaa yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirikia jambo hili? Je, tumekula kitu cho chote cha mfalme? Je, tumejichukulia kitu cho chote kwa ajili yetu wenyewe?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wote wa Yuda wakawajibu watu wa Israeli, “Tulifanya hivi kwa sababu mfalme ni jamaa yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirikia jambo hili? Je, tumekula kitu chochote cha mfalme? Je, tumejichukulia kitu chochote kwa ajili yetu wenyewe?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo watu wote wa Yuda wakawajibu hao watu wa Israeli, Ni kwa sababu mfalme ni wa jamaa yetu; mbona basi ninyi mmekasirika kwa ajili ya jambo hili? Je! Sisi tumekula kitu cha mfalme? Ama ametupa sisi zawadi yoyote?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Yuda wakawaambia watu wa Israeli, “Kwa sababu mfalme ni ndugu yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirika kuhusu jambo hili? Je, tumekula chochote wakati wowote kwa gharama ya mfalme? Au je, yeye ametupa zawadi yoyote?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watu wote wa Yuda walipowajibu Waisiraeli: Maana mfalme ni karibu kwetu; kwa sababu gani mnalichafukia jambo hili? Je? Tumekula mali za mfalme? Au ametupa tunzo lo lote?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo watu wote wa Yuda wakawajibu hao watu wa Israeli, Ni kwa sababu mfalme ndiye wa jamaa yetu; mbona basi ninyi mmekasirika kwa ajili ya jambo hili? Je! Sisi tumekula kitu cha mfalme? Ama ametupa sisi zawadi yo yote?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, watu wote wa Israeli wakakuja kwa mufalme na kumwambia: “Kwa nini wandugu zetu watu wa Yuda walikuwa wamekutwaa ukiwa katika njia, wakakuvukisha muto Yordani, wewe na jamaa yako, pamoja na watu wako?”