2 Samuel 19:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe unawapenda wale wanaokuchukia na unawachukia wale wanaokupenda. Umetuonesha waziwazi leo kwamba makamanda na watumishi wako hawana maana kwako. Naona kuwa leo, kama Absalomu angekuwa hai, na sisi sote tungalikuwa tumekufa, wewe ungefurahi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Unawapenda wale wanaokuchukia, na unawachukia wale wanaokupenda. Leo umeonesha wazi kwamba majemadari wako na watu wao hawana maana kwako. Naona kwamba ungefurahi kama Absalomu angekuwa hai leo na sisi sote tuwe tumekufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa unawapenda wakuchukiao, na unawachukia wakupendao. Maana umetangaza leo ya kuwa wakuu na watumishi wako si kitu kwako; maana leo nimetambua hivi; kama Absalomu angaliishi, na sisi sote tungalikufa leo, ingalikuwa vyema machoni pako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe unawapenda wale wanaokuchukia na unawachukia wale wanaokupenda. Umetuonesha waziwazi leo kwamba makamanda na watumishi wako hawana maana kwako. Naona kuwa leo, kama Absalomu angekuwa hai, na sisi sote tungalikuwa tumekufa, wewe ungefurahi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Unawapenda wale wanaokuchukia, na unawachukia wale wanaokupenda. Leo umeonyesha wazi kwamba majemadari wako na watu wao hawana maana kwako. Naona kwamba ungefurahi kama Absalomu angekuwa hai leo na sisi sote tuwe tumekufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Unawapenda wale wanaokuchukia, na unawachukia wale wanaokupenda. Leo umeonyesha wazi kwamba majemadari wako na watu wao hawana maana kwako. Naona kwamba ungefurahi kama Absalomu angekuwa hai leo na sisi sote tuwe tumekufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa unawapenda wakuchukiao, na unawachukia wakupendao. Maana umetangaza leo ya kuwa wakuu na watumishi wako si kitu kwako; maana leo nimetambua hivi; kama Absalomu angalikuwa hai, na sisi sote tungalikuwa wafu leo, ingekuwa vyema machoni pako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe unawapenda wale wanaokuchukia na unawachukia wale wanaokupenda. Umetuonesha waziwazi leo kwamba makamanda na watumishi wako hawana maana kwako. Naona kuwa leo, kama Absalomu angekuwa hai, na sisi sote tungalikuwa tumekufa, wewe ungefurahi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unawapenda wakuchukiao, ukawachukia wakupendao, kwani leo umevitokeza, ya kuwa wakuu na watumishi si kitu kwako, kwani leo nimevitambua hivi: kama Abisalomu angalikuwa mzima, kama sisi sote tungaliuawa, basi, hili jambo lingenyoka machoni pako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa unawapenda wakuchukiao, na unawachukia wakupendao. Maana umetangaza leo ya kuwa wakuu na watumishi wako si kitu kwako; maana leo nimetambua hivi; kama Absalomu angaliishi, na sisi sote tungalikufa leo, ingalikuwa vyema machoni pako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yoabu aliingia katika nyumba ya mufalme, akamwambia: “Leo umetupatisha haya sisi watumishi wako wote ambao leo tumeyaokoa maisha yako, maisha ya watoto wako wanaume, na maisha ya watoto wako wanawake, maisha ya wake zako na maisha ya wahabara zako.