2 Samuel 19:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, mfalme akatoka akaenda, akaketi mahali pake karibu na lango. Watu wote walipoambiwa kuwa mfalme yuko langoni, wote walimwendea. Wakati huo, watu wote wa Israeli walikuwa wamekimbia, kila mmoja nyumbani kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, mfalme akaondoka na kuketi kwenye kiti chake langoni. Watu walipoambiwa, “Mfalme ameketi langoni,” watu wote wakamjia. Wakati huo, Waisraeli walikuwa wamekimbilia nyumbani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme akaondoka, akaketi langoni. Nao wote wakaambiwa ya kwamba, Angalieni, mfalme ameketi langoni; watu wote wakaenda huko mbele ya mfalme. Basi, Israeli wote walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, mfalme akatoka akaenda, akaketi mahali pake karibu na lango. Watu wote walipoambiwa kuwa mfalme yuko langoni, wote walimwendea. Wakati huo, watu wote wa Israeli walikuwa wamekimbia, kila mmoja nyumbani kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo mfalme akaondoka akaketi kitini pake penye lango. Watu walipoambiwa, “Mfalme ameketi langoni,” watu wote wakamjia. Wakati huo, Waisraeli walikuwa wamekimbilia nyumbani kwao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo mfalme akaondoka akaketi kitini pake penye lango. Watu walipoambiwa, “Mfalme ameketi langoni,” watu wote wakamjia. Wakati huo, Waisraeli walikuwa wamekimbilia nyumbani kwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mfalme akaondoka, akaketi langoni. Nao wote wakaambiwa ya kwamba, Angalieni, mfalme ameketi langoni; watu wote wakaenda huko mbele ya mfalme. Basi, Israeli wote walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, mfalme akatoka akaenda, akaketi mahali pake karibu na lango. Watu wote walipoambiwa kuwa mfalme yuko langoni, wote walimwendea. Wakati huo, watu wote wa Israeli walikuwa wamekimbia, kila mmoja nyumbani kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipoondoka, akaja kukaa langoni; nao watu walipowatangazia watu wote kwamba: Tazameni, mfalme amekaa langoni, watu wote wakaja kumtokea mfalme. Lakini Waisiraeli walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme akaondoka, akaketi langoni. Nao wote wakaambiwa ya kwamba, Angalieni, mfalme ameketi langoni; watu wote wakaenda huko mbele ya mfalme. Basi, Israeli wote walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, simama uzungumuze na watumishi wako kwa upole. Maana, ninaapa kwa Yawe, kama hauendi kuzungumuza nao, hakuna hata mumoja atakayebaki pamoja nawe leo magaribi. Hili litakuwa jambo baya zaidi kwako kuliko maovu yote yaliyokupata tangu ujana wako mpaka leo.”