2 Samuel 19:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote walikuwa wanashindana wao kwa wao katika makabila yote ya Israeli, wakisema, “Mfalme Daudi alitukomboa mikononi mwa adui zetu, alituokoa mikononi mwa Wafilisti. Lakini sasa ameikimbia nchi, akimkimbia Absalomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika makabila yote ya Israeli, watu walikuwa wanabishana wao kwa wao, wakisema, “Mfalme alituokoa kutoka mikononi mwa adui zetu; ndiye alituokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti. Lakini sasa mfalme ameikimbia nchi kwa sababu ya Absalomu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakashindana watu wote katika kabila zote za Israeli, wakisema, Mfalme alitutoa mikononi mwa adui zetu, akatuokoa mikononi mwa Wafilisti; naye sasa amekimbia kutoka nchi hii mbele ya Absalomu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote walikuwa wanashindana wao kwa wao katika makabila yote ya Israeli, wakisema, “Mfalme Daudi alitukomboa mikononi mwa adui zetu, alituokoa mikononi mwa Wafilisti. Lakini sasa ameikimbia nchi, akimkimbia Absalomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika makabila yote ya Israeli, watu walikuwa wanabishana wao kwa wao, wakisema, “Mfalme alituokoa kutoka mikononi mwa adui zetu; yeye ndiye aliyetuokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti. Lakini sasa mfalme ameikimbia nchi kwa sababu ya Absalomu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika makabila yote ya Israeli, watu walikuwa wanabishana wao kwa wao, wakisema, “Mfalme alituokoa kutoka mikononi mwa adui zetu; ndiye alituokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti. Lakini sasa mfalme ameikimbia nchi kwa sababu ya Absalomu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakashindana watu wote katika kabila zote za Israeli, wakisema, Mfalme alitutoa mikononi mwa adui zetu, akatuokoa mikononi mwa Wafilisti; naye sasa amekimbia kutoka nchi hii kwa sababu ya Absalomu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote walikuwa wanashindana wao kwa wao katika makabila yote ya Israeli, wakisema, “Mfalme Daudi alitukomboa mikononi mwa adui zetu, alituokoa mikononi mwa Wafilisti. Lakini sasa ameikimbia nchi, akimkimbia Absalomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wote wakarudiana katika mashina yote ya Waisiraeli kwamba: Mfalme ametuponya mikononi mwa adui zetu, naye ndiye aliyetuponya mikononi mwa Wafilisti, naye hakuwa na budi kumkimbia Abisalomu na kutoka katika nchi hii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakashindana watu wote katika kabila zote za Israeli, wakisema, Mfalme alitutoa mikononi mwa adui zetu, akatuokoa mikononi mwa Wafilisti; naye sasa amekimbia kutoka nchi hii mbele ya Absalomu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, mufalme akatoka, akaenda, akaikaa kwenye nafasi yake karibu na mulango. Watu wote walipoambiwa kwamba mufalme yuko kwenye mulango, wote walimwendea. Wakati ule, watu wote wa Israeli walikuwa wamekimbia, kila mumoja kwake.