2 Samuel 2:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya mambo haya, Daudi alimwomba Mwenyezi-Mungu shauri, akasema, “Je, niende kwenye mji mmojawapo wa miji ya Yuda?” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda!” Daudi akamwuliza, “Niende mji upi?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nenda kwenye mji wa Hebroni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa baada ya mambo haya, Daudi akamuuliza Mwenyezi Mungu, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?” Mwenyezi Mungu akasema, “Panda.” Daudi akauliza, “Je, niende wapi?” Mwenyezi Mungu akajibu, “Nenda Hebroni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Niupandie mji wo wote wa Yuda? Bwana akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya mambo haya, Daudi alimwomba Mwenyezi-Mungu shauri, akasema, “Je, niende kwenye mji mmojawapo wa miji ya Yuda?” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda!” Daudi akamwuliza, “Niende mji upi?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nenda kwenye mji wa Hebroni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa baada ya mambo haya, Daudi akamwuliza BWANA, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?” BWANA akasema, “Panda.” Daudi akauliza, “Je, niende wapi?” BWANA akajibu, “Nenda Hebroni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa baada ya mambo haya, Daudi akamuuliza bwana, “Je, nipande kwenda katika mojawapo ya miji ya Yuda?” bwana akasema, “Panda.” Daudi akauliza, “Je, niende wapi?” bwana akajibu, “Nenda Hebroni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Niupandie mji wowote wa Yuda? BWANA akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya mambo haya, Daudi alimwomba Mwenyezi-Mungu shauri, akasema, “Je, niende kwenye mji mmojawapo wa miji ya Yuda?” Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda!” Daudi akamwuliza, “Niende mji upi?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nenda kwenye mji wa Hebroni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, Dawidi alipomwuliza Bwana baadaye kwamba: Nipande kukaa katika mji mmoja wa Yuda? Bwana akamwambia: Panda! Dawidi akauliza tena: Nipande kukaa wapi? Akamwambia: Heburoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa baada ya hayo, Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Niupandie mji wo wote wa Yuda? BWANA akamwambia, Haya! Panda. Daudi akasema, Niupandie mji upi? Akasema, Hebroni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya mambo yale, Daudi alimwomba Yawe shauri, akasema: “Niende kwenye muji mumoja kati ya miji ya Yuda?” Yawe akamwambia: “Kwenda!” Daudi akamwuliza: “Niende katika muji gani?” Yawe akamujibu: “Kwenda kwenye muji wa Hebroni.”