2 Samuel 2:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ishboshethi alikuwa na umri wa miaka arubaini alipoanza kuitawala Israeli, naye alitawala kwa muda wa miaka miwili. Lakini kabila la Yuda lilimfuata Daudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ish-Boshethi mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
(Huyo Ishboshethi, mwana wa Sauli, umri wake alikuwa amepata miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili.) Lakini nyumba ya Yuda waliandamana na Daudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ishboshethi alikuwa na umri wa miaka arubaini alipoanza kuitawala Israeli, naye alitawala kwa muda wa miaka miwili. Lakini kabila la Yuda lilimfuata Daudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ish-Boshethi mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ish-Boshethi mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala Israeli, naye akatawala miaka miwili. Hata hivyo, nyumba ya Yuda ikamfuata Daudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
(Huyo Ishboshethi, mwana wa Sauli, alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili.) Lakini nyumba ya Yuda waliandamana na Daudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ishboshethi alikuwa na umri wa miaka arubaini alipoanza kuitawala Israeli, naye alitawala kwa muda wa miaka miwili. Lakini kabila la Yuda lilimfuata Daudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Isiboseti, mwana wa Sauli, alikuwa mwenye miaka 40 alipoupata ufalme wa Waisiraeli, akawa mfalme miaka 2; ni wao wa mlango wa Yuda tu waliomfuata Dawidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
(Huyo Ishboshethi, mwana wa Sauli, umri wake alikuwa amepata miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili.) Lakini nyumba ya Yuda waliandamana na Daudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Isiboseti alikuwa na umri wa miaka makumi ine alipoanza kuitawala Israeli, naye alitawala kwa muda wa miaka miwili. Lakini kabila la Yuda lilimufuata Daudi.