2 Samuel 2:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wengine wa Daudi, nao walitoka na kukutana na Abneri na watu aliokuwa nao kwenye bwawa lililoko huko Gibeoni. Kikosi kimoja upande mmoja wa bwawa na kingine upande mwingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wa Daudi wakatoka na kukutana nao kwenye bwawa la Gibeoni. Kikundi kimoja kiliketi upande mmoja wa bwawa, na kikundi kingine upande wa pili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo Yoabu naye, mwana wa Seruya, na watumishi wa Daudi, wakatoka, wakakutana nao karibu na ziwa la Gibeoni; wakaketi, hawa upande huu wa ziwa, na hawa upande huu wa ziwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wengine wa Daudi, nao walitoka na kukutana na Abneri na watu aliokuwa nao kwenye bwawa lililoko huko Gibeoni. Kikosi kimoja upande mmoja wa bwawa na kingine upande mwingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yaobu mwana wa Seruya na watu wa Daudi wakatoka na kukutana nao kwenye bwawa la Gideoni. Kikundi kimoja kiliketi upande mmoja wa bwawa na kikundi kingine upande wa pili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yoabu mwana wa Seruya na watu wa Daudi wakatoka na kukutana nao kwenye bwawa la Gibeoni. Kikundi kimoja kiliketi upande mmoja wa bwawa, na kikundi kingine upande wa pili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo Yoabu naye, mwana wa Seruya, na watumishi wa Daudi, wakatoka, wakakutana nao karibu na ziwa la Gibeoni; wakaketi, hawa upande huu wa ziwa, na hawa upande huu wa ziwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wengine wa Daudi, nao walitoka na kukutana na Abneri na watu aliokuwa nao kwenye bwawa lililoko huko Gibeoni. Kikosi kimoja upande mmoja wa bwawa na kingine upande mwingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yoabu, mwana wa Seruya, alipotoka naye na watumishi wake Dawidi, wakakutana penye ziwa la Gibeoni; hao wakakaa ng'ambo ya huku ya hilo ziwa, nao wale wakakaa ng'ambo ya pili ya hilo ziwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo Yoabu naye, mwana wa Seruya, na watumishi wa Daudi, wakatoka, wakakutana nao karibu na ziwa la Gibeoni; wakaketi, hawa upande huu wa ziwa, na hawa upande huu wa ziwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoabu mwana wa Zeruya na watumishi wengine wa Daudi, nao walitoka na kukutana na Abeneri na watu aliokuwa nao kwenye kiziwa kinachokuwa kule Gibeoni. Kikundi kimoja kikajipanga upande mumoja wa kiziwa na kingine upande mwingine.