2 Samuel 2:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mmoja alimkamata adui yake kichwani, akamchoma mpinzani wake upanga, hivyo wote wawili wakaanguka chini, wamekufa. Hivyo, mahali hapo pakaitwa Helkath-hazurimu. Mahali hapo pako huko Gibeoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kila mwanaume akamkamata mpinzani wake kichwani na kumchoma kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakakamatana, kila mtu akimshika mwenziwe kichwa chake, na kutia upanga wake katika ubavu wa mwenzake; wakaanguka pamoja; hata mahali pale pakaitwa Helkath-hasurimu, napo ni katika Gibeoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mmoja alimkamata adui yake kichwani, akamchoma mpinzani wake upanga, hivyo wote wawili wakaanguka chini, wamekufa. Hivyo, mahali hapo pakaitwa Helkath-hazurimu. Mahali hapo pako huko Gibeoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha kila mtu akakamatana na mpinzani wake kichwani na kuchomana kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha kila mtu akakamatana na mpinzani wake kichwani na kuchomana kwa upanga, nao wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale katika Gibeoni pakaitwa Helkath-Hasurimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakakamatana, kila mtu akimshika mwenziwe kichwa chake, na kutia upanga wake katika ubavu wa mwenzake; wakaanguka pamoja; hata mahali pale pakaitwa Helkath-hasurimu, napo ni katika Gibeoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mmoja alimkamata adui yake kichwani, akamchoma mpinzani wake upanga, hivyo wote wawili wakaanguka chini, wamekufa. Hivyo, mahali hapo pakaitwa Helkath-hazurimu. Mahali hapo pako huko Gibeoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakakamatana kila mtu kichwa cha mwenzake, wakachomana panga kila mtu ubavuni mwa mwenzake, kwa hiyo wakaanguka wote pia, wakafa. Wakapaita mahali pale Fungu lenye Mapanga Makali lililoko Gibeoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakakamatana, kila mtu akimshika mwenziwe kichwa chake, na kutia upanga wake katika ubavu wa mwenzake; wakaanguka pamoja; hata mahali pale pakaitwa Helkath-hasurimu, napo ni katika Gibeoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mumoja alimukamata adui yake kwenye kichwa, na kumuchoma upanga katika ubavu. Hivyo wote wawili wakaanguka chini, wamekufa. Kwa hiyo, pahali pale pakaitwa Shamba la Mapanga. Pahali pale pako kule Gibeoni.