2 Samuel 2:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asaheli alimfuatia Abneri moja kwa moja bila kugeuka kulia wala kushoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati alimfuata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kuume wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asaheli alimfuatia Abneri moja kwa moja bila kugeuka kulia wala kushoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Asaheli akamfukuza Abneri, pasipo kugeuka kulia wala kushoto wakati akimfuata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kulia wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asaheli alimfuatia Abneri moja kwa moja bila kugeuka kulia wala kushoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Asaheli akamkimbiza Abineri na kumfuata, hakujielekeza kwenda kuumeni wala kushotoni, asiache kumfuata Abineri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kuume wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Asaeli alimufuatilia Abeneri moja kwa moja bila kugeuka upande wa kuume wala kushoto.