2 Samuel 2:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abneri akamwambia, “Geukia kulia au kushoto, umkamate kijana mmoja na kuchukua nyara zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfuatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Abneri akamwambia, “Geuka upande wa kulia au kushoto. Mchukue mmoja wa vijana, umvue silaha zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfukuza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kuume au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abneri akamwambia, “Geukia kulia au kushoto, umkamate kijana mmoja na kuchukua nyara zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfuatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Abneri akamwambia, “Geuka upande wa kulia au kushoto. Mchukue mmoja wa vijana wa kiume na umvue silaha zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfukuza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Abneri akamwambia, “Geuka upande wa kulia au kushoto. Mchukue mmoja wa vijana wa kiume na umvue silaha zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfukuza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kulia au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abneri akamwambia, “Geukia kulia au kushoto, umkamate kijana mmoja na kuchukua nyara zake.” Lakini Asaheli hakuacha kumfuatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Abineri akamwambia: Geuka kuumeni kwako au kushotoni kwako, ukamate kijana mmoja, uchukue mata yake! Lakini Asaheli akakataa kuondoka kwake na kuacha kumfuata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kuume au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abeneri akamwambia: “Geukia upande wa kuume au kushoto, umukamate kijana mumoja na kutwaa vitu vyake.” Lakini Asaeli hakuacha kumufuatilia.