2 Samuel 2:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, Mwenyezi-Mungu awafadhili na kuwa mwaminifu kwenu. Nami nitawatendea mema kutokana na jambo mlilolitenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa Mwenyezi Mungu na awaoneshe wema na uaminifu, nami pia nitawaonesha wema ule ule kwa kuwa mmefanya jambo hili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana naye sasa awatendee ninyi fadhili na kweli; mimi nami nitawalipeni fadhili hiyo, kwa sababu mmetenda jambo hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, Mwenyezi-Mungu awafadhili na kuwa mwaminifu kwenu. Nami nitawatendea mema kutokana na jambo mlilolitenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa BWANA na awaonyeshe wema na uaminifu, nami pia nitawaonyesha wema ule ule kwa kuwa mmefanya jambo hili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa bwana na awaonyeshe wema na uaminifu, nami pia nitawaonyesha wema ule ule kwa kuwa mmefanya jambo hili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA naye sasa awatendee ninyi fadhili na kweli; mimi nami nitawalipeni fadhili hiyo, kwa sababu mmetenda jambo hilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, Mwenyezi-Mungu awafadhili na kuwa mwaminifu kwenu. Nami nitawatendea mema kutokana na jambo mlilolitenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa Bwwana na awafanyizie nanyi matendo yanayoelekea kuwa mema kweli, mimi nami na niwarudishie wema huo, kwa kuwa mmefanya jambo hilo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA naye sasa awatendee ninyi fadhili na kweli; mimi nami nitawalipeni fadhili hiyo, kwa sababu mmetenda jambo hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, Yawe awatendee kwa wema na uaminifu. Nami nitawatendea vizuri kutokana na jambo mulilolitenda.