2 Samuel 2:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini muwe imara na mashujaa. Shauli, bwana wenu, amekufa, na watu wa Yuda wamenipaka mafuta niwe mfalme wao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa basi, kuweni hodari na mashujaa, kwa maana bwana wenu Sauli amekufa, nao watu wa nyumba ya Yuda wamenipaka mafuta niwe mfalme juu yao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa, mikono yenu na itiwe nguvu, nanyi iweni mashujaa; maana Sauli, bwana wenu, amekufa, tena nyumba ya Yuda wamenitia mimi mafuta niwe mfalme juu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini muwe imara na mashujaa. Shauli, bwana wenu, amekufa, na watu wa Yuda wamenipaka mafuta niwe mfalme wao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa basi, iweni hodari na mashujaa, kwa maana bwana wenu Sauli amekufa, nayo nyumba ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme juu yao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa basi, kuweni hodari na mashujaa, kwa maana bwana wenu Sauli amekufa, nayo nyumba ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme juu yao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa, mikono yenu na itiwe nguvu, nanyi iweni mashujaa; maana Sauli, bwana wenu, amekufa, tena nyumba ya Yuda wamenitia mimi mafuta niwe mfalme wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini muwe imara na mashujaa. Shauli, bwana wenu, amekufa, na watu wa Yuda wamenipaka mafuta niwe mfalme wao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa na mwikaze mikono yenu, mpate nguvu, kwani bwana wenu Sauli amekufa, tena mimi nami wao wa mlango wa Yuda wamenipaka mafuta, niwe mfalme wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa, mikono yenu na itiwe nguvu, nanyi iweni mashujaa; maana Sauli, bwana wenu, amekufa, tena nyumba ya Yuda wamenitia mimi mafuta niwe mfalme juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mukuwe imara na mashujaa. Saulo, bwana wenu, amekufa, na watu wa Yuda wamenipakaa mafuta nikuwe mufalme wao.”