2 Samuel 20:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa ikawa kwamba huko Gilgali kulikuwa na mtu mmoja mlaghai aitwaye Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini. Basi Sheba alipiga tarumbeta, na kusema, “Hatuna fungu lolote kwa Daudi, hatuna sehemu yetu katika huyo mwana wa Yese. Enyi watu wa Israeli, kila mmoja na ajiendee hemani kwake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi, kulikuwa na mtu mbaya sana aliyeitwa Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini, aliyekuwako huko. Akapiga tarumbeta na kupaza sauti, “Hatuna fungu katika Daudi, wala hatuna sehemu katika mwana wa Yese! Kila mtu aende kwenye hema lake, enyi Israeli!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa ikawa kwamba huko Gilgali kulikuwa na mtu mmoja mlaghai aitwaye Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini. Basi Sheba alipiga tarumbeta, na kusema, “Hatuna fungu lolote kwa Daudi, hatuna sehemu yetu katika huyo mwana wa Yese. Enyi watu wa Israeli, kila mmoja na ajiendee hemani kwake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi, kulikuwa na mtu mbaya sana aliyeitwa Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini, aliyekuwako huko. Akapiga tarumbeta na kupaza sauti, “Hatuna fungu katika Daudi, wala hatuna sehemu katika mwana wa Yese! Kila mtu aende hemani mwake, Enyi Israeli!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi, kulikuwa na mtu mbaya sana aliyeitwa Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini, aliyekuwako huko. Akapiga tarumbeta na kupaza sauti, “Hatuna fungu katika Daudi, wala hatuna sehemu katika mwana wa Yese! Kila mtu aende hemani mwake, enyi Israeli!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa ikawa kwamba huko Gilgali kulikuwa na mtu mmoja mlaghai aitwaye Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini. Basi Sheba alipiga tarumbeta, na kusema, “Hatuna fungu lolote kwa Daudi, hatuna sehemu yetu katika huyo mwana wa Yese. Enyi watu wa Israeli, kila mmoja na ajiendee hemani kwake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikatukia, ya kama kulikuwa na mtu asiyefaa, jina lake Seba, mwana wa Bikri, mtu wa Benyamini. Akapiga baragumu kwamba: Sisi hatuna fungu kwake Dawidi, wala hatuna lililo letu kwake mwana wa Isai. Ninyi Waisiraeli, kila mtu na aende hemani kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa ilitokea kwamba kule Gilgali kulikuwa mutu mumoja wa ovyoovyo anayeitwa Seba mwana wa Bikiri, wa kabila la Benjamina. Basi Seba alipiga baragumu, na kusema: “Hatuna ushirika wowote na Daudi; hatuna sehemu yetu katika huyo mwana wa Yese. Enyi watu wa Israeli, kila mumoja ajiendee katika hema yake!”