2 Samuel 20:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Amasa hakuona upanga uliokuwa mkononi mwa Yoabu. Basi, Yoabu akamchoma Amasa upanga tumboni, matumbo yake yakatoka nje, akafa. Yoabu hakumchoma upanga mara mbili. Kisha, Yoabu na nduguye Abishai wakaendelea kumfuatilia Sheba mwana wa Bikri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amasa hakuona upanga uliokuwa mkononi mwa Yoabu, naye Yoabu akamchoma nao tumboni, nayo matumbo yake yakamwagika chini. Pasipo kuchomwa mara ya pili, Amasa akafa. Basi Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao wa tumbo, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Amasa hakuona upanga uliokuwa mkononi mwa Yoabu. Basi, Yoabu akamchoma Amasa upanga tumboni, matumbo yake yakatoka nje, akafa. Yoabu hakumchoma upanga mara mbili. Kisha, Yoabu na nduguye Abishai wakaendelea kumfuatilia Sheba mwana wa Bikri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amasa hakuona upanga uliokuwa mkononi mwa Yoabu, naye Yoabu akamchoma nao tumboni, nayo matumbo yake yakamwagika chini. Pasipo kuchomwa mara ya pili, Amasa akafa. Basi Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amasa hakuona upanga uliokuwa mkononi mwa Yoabu, naye Yoabu akamchoma nao tumboni, nayo matumbo yake yakamwagika chini. Pasipo kuchomwa mara ya pili, Amasa akafa. Basi Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao tumboni, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Amasa hakuona upanga uliokuwa mkononi mwa Yoabu. Basi, Yoabu akamchoma Amasa upanga tumboni, matumbo yake yakatoka nje, akafa. Yoabu hakumchoma upanga mara mbili. Kisha, Yoabu na nduguye Abishai wakaendelea kumfuatilia Sheba mwana wa Bikri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amasa asipouangalia upanga uliomo mkononi mwa Yoabu, akamchoma nao tumboni, matumbo yake yamwagike chini, hakumchoma mara ya pili, akafa tu. Kisha Yoabu na ndugu yake Abisai wakaenda kumfukuza Seba, mwana wa Bikri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao wa tumbo, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Amasa hakuona upanga uliokuwa katika mukono wa Yoabu. Basi, Yoabu akamuchoma Amasa upanga ndani ya tumbo, matumbotumbo yake yakatoka inje, akakufa. Yoabu hakumuchoma upanga mara mbili. Kisha, Yoabu na ndugu yake Abisayi wakaendelea kumufuatilia Seba mwana wa Bikiri.