2 Samuel 20:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakaenda kumzingira Sheba akiwa katika mji huo wa Abeli wa Beth-maaka. Walirundika kuuzingira mji, na ngome; halafu wakaanza kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vikosi vyote vya Yoabu vikaja na kumzingira Sheba mwana wa Bikri huko Abel-Beth-Maaka. Wakauzingira mji kwa kuweka vikosi vya askari, ili kukabiliana na ngome ya mji. Walipokuwa wakijaribu kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao wakaja wakamhusuru katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya chuguu mbele ya mji, nayo ikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunja-vunja ukuta, wapate kuubomoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakaenda kumzingira Sheba akiwa katika mji huo wa Abeli wa Beth-maaka. Walirundika kuuzingira mji, na ngome; halafu wakaanza kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vikosi vyote vya Yoabu vikaja na kumhusuru Sheba mwana wa Bikri huko Abeli ya Beth-Maaka. Wakauzingira mji kwa kuweka vikosi vya askari, ili kukabiliana na ngome ya Mji. Walipokuwa wanagongagonga ukuta ili kuubomoa na kuuangusha chini,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vikosi vyote vya Yoabu vikaja na kumhusuru Sheba mwana wa Bikri huko Abel-Beth-Maaka. Wakauzingira mji kwa kuweka vikosi vya askari, ili kukabiliana na ngome ya mji. Walipokuwa wanagongagonga ukuta ili kuubomoa na kuuangusha chini,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao wakaja wakauzingira katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya kilima mbele ya mji, nacho kikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunjavunja ukuta, wapate kuubomoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakaenda kumzingira Sheba akiwa katika mji huo wa Abeli wa Beth-maaka. Walirundika kuuzingira mji, na ngome; halafu wakaanza kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wale walipokuja wakamsonga na kumzinga kule Abeli kwa Beti-Maka, wakiujengea mji huo boma la mchanga la kuuzunguka, nalo kikasimama papo hapo, mfereji wa boma la mji ulipokuwa. Nao watu wote waliokuwa na Yoabu wakachimba chini ya ukuta wa boma lao, wauangushe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao wakaja wakamhusuru katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya chuguu mbele ya mji, nayo ikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunja-vunja ukuta, wapate kuubomoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakaenda kumuzunguka Seba akiwa katika muji ule wa Abeli wa Beti-Maka. Walilundika udongo kwa kuzunguka muji, na makimbilio. Halafu wakaanza kuubomoa ukuta kwa kuuangusha chini.