2 Samuel 20:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulivyosema si kweli! Lakini mtu mmoja kutoka sehemu ya milima ya Efraimu aitwaye Sheba mwana wa Bikri anataka kumwasi mfalme Daudi. Mtoeni huyo kwangu nami nitaondoka mjini kwenu.” Yule mwanamke akamwambia Yoabu, “Kichwa chake kitarushwa kwako kupitia ukutani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo sivyo ilivyo. Mtu mmoja jina lake Sheba mwana wa Bikri, kutoka nchi ya vilima ya Efraimu, ameinua mkono wake dhidi ya mfalme, dhidi ya Daudi. Mkabidhini mtu huyu mmoja kwangu, nami nitajiondoa katika mji huu.” Huyu mwanamke akamwambia Yoabu, “Kichwa chake mtatupiwa kupitia juu ya ukuta.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, Sheba, mwana wa Bikri, jina lake, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulivyosema si kweli! Lakini mtu mmoja kutoka sehemu ya milima ya Efraimu aitwaye Sheba mwana wa Bikri anataka kumwasi mfalme Daudi. Mtoeni huyo kwangu nami nitaondoka mjini kwenu.” Yule mwanamke akamwambia Yoabu, “Kichwa chake kitarushwa kwako kupitia ukutani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo sivyo ilivyo. Mtu mmoja jina lake Sheba mwana wa Bikri, kutoka nchi ya vilima vya Efraimu, ameinua mkono wake dhidi ya mfalme, dhidi ya Daudi. Nikabidhini mtu huyu mmoja, nami nitajiondoa katika mji huu.” Huyu mwanamke akamwambia Yoabu, “Kichwa chake mtatupiwa kupitia juu ya ukuta.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo sivyo ilivyo. Mtu mmoja jina lake Sheba mwana wa Bikri, kutoka nchi ya vilima vya Efraimu, ameinua mkono wake dhidi ya mfalme, dhidi ya Daudi. Nikabidhini mtu huyu mmoja, nami nitajiondoa katika mji huu.” Huyu mwanamke akamwambia Yoabu, “Kichwa chake mtatupiwa kupitia juu ya ukuta.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, jina lake, Sheba, mwana wa Bikri, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulivyosema si kweli! Lakini mtu mmoja kutoka sehemu ya milima ya Efraimu aitwaye Sheba mwana wa Bikri anataka kumwasi mfalme Daudi. Mtoeni huyo kwangu nami nitaondoka mjini kwenu.” Yule mwanamke akamwambia Yoabu, “Kichwa chake kitarushwa kwako kupitia ukutani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi haviko kabisa, ila yuko mtoro wa milima ya Efuraimu, jina lake Seba, mwana wa Bikri; huyu ameuinua mkono wake, amwue mfalme Dawidi. Mtoeni huyu peke yake tu! Ndipo, nitakapoondoka penye mji huu. Naye yule mwanamke akamwambia Yoabu: Utakiona kichwa chake, kikitupwa kwako toka ukutani juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, Sheba, mwana wa Bikri, jina lake, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ulivyosema si kweli! Lakini mutu mumoja kutoka sehemu ya milima ya Efuraimu anayeitwa Seba mwana wa Bikiri anataka kumwasi mufalme Daudi. Mumutoe kwangu nami nitaondoka katika muji wenu.” Yule mwanamuke akamwambia Yoabu: “Kichwa chake kitarushwa kwako kupitia juu ya ukuta.”