2 Samuel 20:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwambia Abishai, “Sasa, Sheba mwana wa Bikri, atatuletea madhara kuliko Absalomu. Chukua watumishi wangu, umfuatie Sheba asije akaingia kwenye miji yenye ngome akaponyoka, tusimwone tena.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatuletea madhara kuliko Absalomu. Wachukue watumishi wa bwana wako na umfuatie, la sivyo atapata mji wenye ngome na kututoroka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Daudi akamwambia Abishai, Sasa Sheba, mwana wa Bikri, atatudhuru, kuliko Absalomu; twaa wewe watumishi wa bwana wako, ukamfuatie, asiingie katika miji yenye boma, na kujiponya machoni petu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwambia Abishai, “Sasa, Sheba mwana wa Bikri, atatuletea madhara kuliko Absalomu. Chukua watumishi wangu, umfuatie Sheba asije akaingia kwenye miji yenye ngome akaponyoka, tusimwone tena.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatuletea madhara zaidi kuliko alivyofanya Absalomu. Wachukue watu wa bwana wako na umfuatie, la sivyo atapata mji wenye ngome na kututoroka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatuletea madhara zaidi kuliko alivyofanya Absalomu. Wachukue watu wa bwana wako na umfuatie, la sivyo atapata mji wenye ngome na kututoroka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Daudi akamwambia Abishai, Sasa Sheba, mwana wa Bikri, atatudhuru, kuliko Absalomu; twaa wewe watumishi wa bwana wako, ukamfuatie, asiingie katika miji yenye boma, na kutuponyoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwambia Abishai, “Sasa, Sheba mwana wa Bikri, atatuletea madhara kuliko Absalomu. Chukua watumishi wangu, umfuatie Sheba asije akaingia kwenye miji yenye ngome akaponyoka, tusimwone tena.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akamwambia Abisai: Sasa Seba, mwana wa Bikri, atatupatia mabaya kuliko Abisalomu; wewe wachukue watumishi wa bwana wako, umfukuze, asijipatie miji yenye maboma ya kuponea humo, macho yetu yasimwone tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Daudi akamwambia Abishai, Sasa Sheba, mwana wa Bikri, atatudhuru, kuliko Absalomu; twaa wewe watumishi wa bwana wako, ukamfuatie, asiingie katika miji yenye boma, na kujiponya machoni petu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwambia Abisayi: “Sasa, Seba mwana wa Bikiri, atatuletea taabu kuliko Abusaloma. Twaa watumishi wangu, umufuate Seba kusudi asiingie kwenye miji yenye kuta na kuponyoka tusimwone tena.”