2 Samuel 20:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipofika kwenye jiwe kubwa lililoko huko Gibeoni, Amasa akatoka kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa vazi la kijeshi, na ndani ya vazi hilo kulikuwa na mkanda ulioshikilia upanga kiunoni mwake ukiwa kwenye ala yake. Yoabu alipokuwa anakaribia, upanga wake ulichomoka alani ukaanguka chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa kwenye mwamba mkubwa huko Gibeoni, Amasa alikuja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa mavazi yake ya kijeshi; juu yake alifunga mkanda kiunoni wenye upanga ndani ya ala. Alipokuwa akienda mbele, ule upanga ukaanguka kutoka ala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi walipokuwako kwenye lile jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Naye Yoabu alikuwa amefungwa mavazi yake ya vita aliyoyavaa, na juu yake alikuwa na mshipi, na upanga uliotiwa viunoni mwake ndani ya ala yake; naye alipokuwa akiendelea, ukaanguka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipofika kwenye jiwe kubwa lililoko huko Gibeoni, Amasa akatoka kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa vazi la kijeshi, na ndani ya vazi hilo kulikuwa na mkanda ulioshikilia upanga kiunoni mwake ukiwa kwenye ala yake. Yoabu alipokuwa anakaribia, upanga wake ulichomoka alani ukaanguka chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati walipokuwa kwenye mwamba mkubwa huko Gibeoni, Amasa alikuja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa mavazi yake ya kijeshi; juu yake alifunga mkanda kwenye kiuno wenye upanga ndani ya ala. Alipokuwa akienda mbele, ule upanga ukaanguka kutoka kwenye ala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati walikuwa kwenye mwamba mkubwa huko Gibeoni, Amasa alikuja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa mavazi yake ya kijeshi; juu yake alifunga mkanda kwenye kiuno wenye upanga ndani ya ala. Alipokuwa akienda mbele, ule upanga ukaanguka kutoka kwenye ala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi walipokuwako kwenye lile jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Naye Yoabu alikuwa amefungwa mavazi yake ya vita aliyoyavaa, na juu yake alikuwa na mshipi, na upanga uliotiwa viunoni mwake ndani ya ala yake; naye alipokuwa akienda, ukaanguka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipofika kwenye jiwe kubwa lililoko huko Gibeoni, Amasa akatoka kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa vazi la kijeshi, na ndani ya vazi hilo kulikuwa na mkanda ulioshikilia upanga kiunoni mwake ukiwa kwenye ala yake. Yoabu alipokuwa anakaribia, upanga wake ulichomoka alani ukaanguka chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao walipofika kwenye lile jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akawatokea usoni. Naye Yoabu alikuwa amejifunga nguo zake za vitani, alizozivaa kila mara, juu yao alikuwa amejifunga upanga uliofungwa kiunoni, nao ulikuwa ndani ya ala yake; lakini alipokwenda huko na huko, ukaanguka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi walipokuwako kwenye lile jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Naye Yoabu alikuwa amefungwa mavazi yake ya vita aliyoyavaa, na juu yake alikuwa na mshipi, na upanga uliotiwa viunoni mwake ndani ya ala yake; naye alipokuwa akiendelea, ukaanguka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika kwenye jiwe kubwa linalokuwa kule Gibeoni, Amasa akatoka kwenda kuwapokea. Yoabu alikuwa akivaa nguo ya kiaskari, na ndani ya nguo ile kulikuwa mukaba ulioshikilia upanga kwenye kiuno chake ukiwa kwenye mufuko wake. Yoabu alipokuwa anakaribia, upanga wake ulichomoka ndani ya mufuko ukaanguka chini.