2 Samuel 21:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati mmoja kulitokea njaa kali nchini Daudi akiwa mfalme. Njaa hiyo ilidumu miaka mitatu mfululizo. Daudi alimwomba Mwenyezi-Mungu shauri. Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Shauli na jamaa yake wana hatia ya kumwaga damu kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa utawala wa Daudi kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu mfululizo, kwa hiyo Daudi akautafuta uso wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akasema, “Ni kwa sababu ya Sauli na nyumba yake iliyotiwa madoa ya damu, kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati mmoja kulitokea njaa kali nchini Daudi akiwa mfalme. Njaa hiyo ilidumu miaka mitatu mfululizo. Daudi alimwomba Mwenyezi-Mungu shauri. Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Shauli na jamaa yake wana hatia ya kumwaga damu kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa utawala wa Daudi kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu mfululizo, kwa hiyo Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, “Ni kwa sababu ya Sauli na nyumba yake iliyotiwa madoa ya damu, kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa utawala wa Daudi kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu mfululizo, kwa hiyo Daudi akautafuta uso wa bwana. bwana akasema, “Ni kwa sababu ya Sauli na nyumba yake iliyotiwa madoa ya damu, kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati mmoja kulitokea njaa kali nchini Daudi akiwa mfalme. Njaa hiyo ilidumu miaka mitatu mfululizo. Daudi alimwomba Mwenyezi-Mungu shauri. Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Shauli na jamaa yake wana hatia ya kumwaga damu kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika siku za Dawidi kulikuwa na njaa mwaka kwa mwaka, miaka mitatu; naye Dawidi alipoutafuta uso wa Bwana, Bwana akasema: Ziko manza za damu, Sauli nao wa mlango wake walizozikora walipowaua watu wa Gibeoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati mumoja katika siku za utawala wa Daudi kukatokea njaa kali katika inchi. Njaa hiyo ilidumu miaka mitatu yenye kufuatana. Daudi alimwomba Yawe shauri. Yawe akamwambia: “Saulo na jamaa yake wana makosa ya kumwanga damu kwa sababu aliwaua Wagibeoni.”