2 Samuel 21:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Rispa binti Aya alichukua nguo ya gunia, akajitandikia mwambani. Alikaa hapo tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati wa mvua ulipowadia na kuinyeshea maiti. Wakati huo wote, aliwafukuza ndege wa angani na wanyama wa porini, usiku na mchana, ili wasifikie maiti hizo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Rispa binti Aya akachukua gunia, akajitandikia juu ya mwamba. Kuanzia mwanzo wa mavuno hadi mvua ziliponyesha juu ya miili ya hao waliouawa, Rispa hakuruhusu ndege wa angani kuwagusa wakati wa mchana, wala wanyama mwitu wakati wa usiku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Rispa binti Aya alichukua nguo ya gunia, akajitandikia mwambani. Alikaa hapo tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati wa mvua ulipowadia na kuinyeshea maiti. Wakati huo wote, aliwafukuza ndege wa angani na wanyama wa porini, usiku na mchana, ili wasifikie maiti hizo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Rispa binti Ahiya akachukua nguo ya gunia, akajitandikia juu ya mwamba. Kuanzia mwanzo wa mavuno mpaka mvua ziliponyesha juu ya miili ya hao waliouawa, Rispa hakuruhusu ndege wa angani kuwagusa wakati wa mchana, wala wanyama wa mwitu wakati wa usiku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Rispa binti Aiya akachukua nguo ya gunia, akajitandikia juu ya mwamba. Kuanzia mwanzo wa mavuno mpaka mvua ziliponyesha juu ya miili ya hao waliouawa, Rispa hakuruhusu ndege wa angani kuwagusa wakati wa mchana, wala wanyama wa mwitu wakati wa usiku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hadi waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Rispa binti Aya alichukua nguo ya gunia, akajitandikia mwambani. Alikaa hapo tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati wa mvua ulipowadia na kuinyeshea maiti. Wakati huo wote, aliwafukuza ndege wa angani na wanyama wa porini, usiku na mchana, ili wasifikie maiti hizo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Risipa, binti Aya, akachukua gunia, akalitandika la kulalia mwambani juu tangu hapo, watu walipoanza kuvuna, mpaka mvua zitokazo mbinguni zikawanyeshea wale wafu, hakuacha ndege wa angani kuwakalia mchana, wala nyama wa porini kuwafikia usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Risipa binti ya Aya alitwaa nguo ya gunia, akajitandikia juu ya jiwe kubwa. Alikaa pale tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati wa mvua ulipofika na kuinyeshea maiti. Wakati huo wote, aliwafukuza ndege na wanyama wa pori, usiku na muchana, kusudi wasifikie maiti hizo.