2 Samuel 21:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alikwenda na kuichukua mifupa ya Shauli na Yonathani mwanawe kutoka wakazi wa Yabesh-gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka mtaani huko Beth-sheani, ambako Wafilisti walikuwa wamemtundika Shauli na Yonathani siku ile Wafilisti walipomuua Shauli mlimani Gilboa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
alienda akachukua mifupa ya Sauli na mwanawe Yonathani kutoka kwa watu wa Yabesh-Gileadi. (Walikuwa wameichukua kwa siri kutoka uwanja wa watu wote huko Beth-Shani, ambapo Wafilisti walikuwa wamewatundika baada ya kumuua Sauli huko Gilboa.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Bethshani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alikwenda na kuichukua mifupa ya Shauli na Yonathani mwanawe kutoka wakazi wa Yabesh-gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka mtaani huko Beth-sheani, ambako Wafilisti walikuwa wamemtundika Shauli na Yonathani siku ile Wafilisti walipomuua Shauli mlimani Gilboa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
alikwenda akachukua mifupa ya Sauli na mwanawe Yonathani kutoka kwa watu wa Yabeshi-Gileadi. (Walikuwa wameichukua kwa siri kutoka katika uwanja wa watu wote huko Beth-Shani, mahali ambapo Wafilisti walikuwa wamewatundika baada ya kumwua Sauli huko Gilboa.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
alikwenda akachukua mifupa ya Sauli na mwanawe Yonathani kutoka kwa watu wa Yabeshi-Gileadi. (Walikuwa wameichukua kwa siri kutoka uwanja wa watu wote huko Beth-Shani, mahali ambapo Wafilisti walikuwa wamewatundika baada ya kumuua Sauli huko Gilboa.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Beth-sheani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alikwenda na kuichukua mifupa ya Shauli na Yonathani mwanawe kutoka wakazi wa Yabesh-gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka mtaani huko Beth-sheani, ambako Wafilisti walikuwa wamemtundika Shauli na Yonathani siku ile Wafilisti walipomuua Shauli mlimani Gilboa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akaenda akaichukua mifupa ya Sauli nayo mifupa ya mwanawe Yonatani kwa wenyeji wa Yabesi wa Gileadi walioiiba uwanjani kwa Beti-Sani; ndiko, Wafilisti walikoitungika siku hiyo, Wafilisti walipomwua Sauli huko Gilboa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Bethshani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alikwenda na kuitwaa mifupa ya Saulo na ya mwana wake Yonatani kutoka kwa wakaaji wa Yabeshi-Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka kule Beti-Sani, ambako Wafilistini walikuwa wamemutundika Saulo na Yonatani siku ile walipomwua Saulo kwenye mulima Gilboa.