2 Samuel 21:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Abishai mwana wa Seruya, alikwenda kumsaidia Daudi. Abishai alimshambulia yule Mfilisti na kumwua. Hivyo, watu wakamwapia Daudi wakisema, “Hutakwenda tena nasi vitani, la sivyo utaizima taa ya ufalme katika Israeli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Abishai mwana wa Seruya akaja kumwokoa Daudi; akampiga huyo Mfilisti, akamwangusha chini na kumuua. Ndipo watu wakamwapia Daudi, wakisema, “Kamwe hutaenda tena nasi vitani, ili taa ya Israeli isije ikazimwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Abishai mwana wa Seruya, alikwenda kumsaidia Daudi. Abishai alimshambulia yule Mfilisti na kumwua. Hivyo, watu wakamwapia Daudi wakisema, “Hutakwenda tena nasi vitani, la sivyo utaizima taa ya ufalme katika Israeli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Abishai mwana wa Seruya akaja kumwokoa Daudi; akampiga huyo Mfilisti, akamwangusha chini na kumwua. Ndipo watu wakamwapia Daudi, wakisema, “Kamwe hutakwenda tena nasi vitani, ili kwamba taa ya Israeli isije ikazimwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Abishai mwana wa Seruya akaja kumwokoa Daudi; akampiga huyo Mfilisti, akamwangusha chini na kumuua. Ndipo watu wakamwapia Daudi, wakisema, “Kamwe hutakwenda tena nasi vitani, ili kwamba taa ya Israeli isije ikazimwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Abishai mwana wa Seruya, alikwenda kumsaidia Daudi. Abishai alimshambulia yule Mfilisti na kumwua. Hivyo, watu wakamwapia Daudi wakisema, “Hutakwenda tena nasi vitani, la sivyo utaizima taa ya ufalme katika Israeli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Abisai, mwana wa Seruya, alipomsaidia na kumpiga yule Mfilisti, hata akafa. Hapo ndipo, watumishi wa Dawidi walipomwapia kwamba: Wewe hutatoka tena pamoja na sisi kwenda vitani, usiizime taa ya waisiraeli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Abisayi mwana wa Zeruya alikwenda kumusaidia Daudi. Abisayi alimushambulia yule Mufilistini na kumwua. Kwa hiyo, watu wakamwapia Daudi wakisema: “Hautakwenda tena nasi katika vita, kusudi usiizime taa ya ufalme katika Israeli.”