2 Samuel 21:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, mfalme Daudi akawaita Wagibeoni (Wagibeoni hawakuwa Waisraeli ila walikuwa mabaki ya Waamori. Ingawa watu wa Israeli walikuwa wameapa kuwaacha hai, lakini Shauli alijaribu kuwaua wote kwani alikuwa na bidii ya upendeleo kwa watu wa Israeli na wa Yuda).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akawaita Wagibeoni na kuzumgumza nao. (Wagibeoni hawakuwa sehemu ya Israeli, ila walikuwa mabaki ya Waamori. Waisraeli walikuwa wameapa kuwaacha hai, lakini Sauli katika wivu wake kwa ajili ya Israeli na Yuda, alikuwa amejaribu kuwaangamiza.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi yake kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, mfalme Daudi akawaita Wagibeoni (Wagibeoni hawakuwa Waisraeli ila walikuwa mabaki ya Waamori. Ingawa watu wa Israeli walikuwa wameapa kuwaacha hai, lakini Shauli alijaribu kuwaua wote kwani alikuwa na bidii ya upendeleo kwa watu wa Israeli na wa Yuda).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akawaita Wagibeoni na kuzumgumza nao. (Wagibeoni hawakuwa wa wana wa Israeli, ila walikuwa mabaki ya Waamori. Waisraeli walikuwa wameapa kuwaacha hai, lakini Sauli katika wivu wake kwa ajili ya Israeli na Yuda, alikuwa amejaribu kuwaangamiza.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akawaita Wagibeoni na kuzumgumza nao. (Wagibeoni hawakuwa wa wana wa Israeli, ila walikuwa mabaki ya Waamori. Waisraeli walikuwa wameapa kuwaacha hai, lakini Sauli katika wivu wake kwa ajili ya Israeli na Yuda, alikuwa amejaribu kuwaangamiza.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akajaribu kuwaua kwa ari kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;)
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, mfalme Daudi akawaita Wagibeoni (Wagibeoni hawakuwa Waisraeli ila walikuwa mabaki ya Waamori. Ingawa watu wa Israeli walikuwa wameapa kuwaacha hai, lakini Shauli alijaribu kuwaua wote kwani alikuwa na bidii ya upendeleo kwa watu wa Israeli na wa Yuda).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipowaita Wagibeoni kusema nao; nao Wagibeoni hawakuwa wana wa Isiraeli, ila walikuwa masao yao Waamori, nao wana wa Isiraeli walikuwa wamefanya maagano nao na kuapa, lakini Sauli alitaka kuwaua kwa kuona wivu kwa ajili ya wana wa Isiraeli na wa Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi yake kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;)
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, mufalme Daudi akawaita Wagibeoni. Wagibeoni hawakukuwa Waisraeli lakini walikuwa mabaki ya Waamori. Watu wa Israeli walikuwa wameapa kuwaacha wazima, lakini Saulo alijaribu kuwaua wote maana alikuwa na bidii ya upendeleo kwa watu wa Israeli na wa Yuda.