2 Samuel 21:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, tukabidhi watu saba kati ya wanawe wa kiume, nasi tuwanyonge mbele ya Mwenyezi-Mungu mlimani Gibea, kwa Shauli aliyeteuliwa na Mwenyezi-Mungu.” Mfalme akasema, “Nitawakabidhi kwenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
tupatieni wazao wake saba wa kiume, tuwaue hadharani mbele za Mwenyezi Mungu huko Gibea ya Sauli, aliyekuwa amechaguliwa na Mwenyezi Mungu.” Basi mfalme akasema, “Nitawakabidhi kwenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za Bwana katika Gibeoni, katika mlima wa Bwana. Mfalme akasema, Nitawatoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, tukabidhi watu saba kati ya wanawe wa kiume, nasi tuwanyonge mbele ya Mwenyezi-Mungu mlimani Gibea, kwa Shauli aliyeteuliwa na Mwenyezi-Mungu.” Mfalme akasema, “Nitawakabidhi kwenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
tupatieni wazao wake saba wa kiume tuwaue hadharani mbele za BWANA huko Gibea ya Sauli, aliyekuwa amechaguliwa na BWANA.” Basi mfalme akasema, “Nitawakabidhi kwenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
tupatieni wazao wake saba wa kiume tuwaue hadharani mbele za bwana huko Gibea ya Sauli, aliyekuwa amechaguliwa na bwana.” Basi mfalme akasema, “Nitawakabidhi kwenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za BWANA katika Gibeoni, katika mlima wa BWANA. Mfalme akasema, Nitawatoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, tukabidhi watu saba kati ya wanawe wa kiume, nasi tuwanyonge mbele ya Mwenyezi-Mungu mlimani Gibea, kwa Shauli aliyeteuliwa na Mwenyezi-Mungu.” Mfalme akasema, “Nitawakabidhi kwenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, na tupewe wanawe saba, tuwanyonge machoni pa Bwana kule Gibea kwa Sauli aliyekuwa mteule wa Bwana. Mfalme akawaambia: Mimi nitawapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za BWANA katika Gibeoni, katika mlima wa BWANA. Mfalme akasema, Nitawatoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, utupatie watu saba kati ya wazao wake, nasi tuwatundike mbele ya Yawe juu ya mulima Gibea, kwa Saulo aliyechaguliwa na Yawe.” Mufalme akasema: “Nitawapatia nao.”