2 Samuel 21:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watoto hao saba wa kiume Daudi aliwakabidhi kwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele ya Mwenyezi-Mungu, wote saba wakafa pamoja. Watoto hao waliuawa mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawakabidhi kwa Wagibeoni, ambao waliwaua na kuwaweka wazi juu ya kilima mbele za Mwenyezi Mungu. Wote saba walianguka kwa pamoja; waliuawa katika siku za kwanza za mavuno, mara tu uvunaji wa shayiri ulipokuwa unaanza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za Bwana, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watoto hao saba wa kiume Daudi aliwakabidhi kwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele ya Mwenyezi-Mungu, wote saba wakafa pamoja. Watoto hao waliuawa mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawakabidhi kwa Wagibeoni, ambao waliwaua na kuwaweka wazi juu ya kilima mbele za BWANA. Wote saba walianguka kwa pamoja; waliuawa katika siku za kwanza za mavuno, mara tu uvunaji wa shayiri ulipokuwa unaanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawakabidhi kwa Wagibeoni, ambao waliwaua na kuwaweka wazi juu ya kilima mbele za bwana. Wote saba walianguka kwa pamoja; waliuawa katika siku za kwanza za mavuno, mara tu uvunaji wa shayiri ulipokuwa unaanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za BWANA, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watoto hao saba wa kiume Daudi aliwakabidhi kwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele ya Mwenyezi-Mungu, wote saba wakafa pamoja. Watoto hao waliuawa mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawanyonga mlimani juu machoni pa Bwana; nao wote saba wakauawa pamoja; walipouawa, ni siku za kwanza za mavuno, watu walipoanza kuvuna mawele.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za BWANA, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi aliwatoa watoto hao saba wanaume kwa Wagibeoni, nao wakawatundika kwenye mulima mbele ya Yawe, wote saba wakakufa pamoja. Watoto hao waliuawa kwa mwanzo wa mavuno ya Shayiri.