2 Samuel 22:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu alipowakemea, kutokana na pumzi ya puani mwake, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Mwenyezi Mungu, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake Bwana, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu alipowakemea, kutokana na pumzi ya puani mwake, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mabonde ya bahari yalifunuliwa na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake BWANA, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake bwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu alipowakemea, kutokana na pumzi ya puani mwake, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, vilipoonekana vilindi vya baharini, nayo misingi ya nchi ikafunuliwa kwa nguvu ya makaripio yake yeye Bwana na kwa ukali wa pumzi ya pua yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe alipovikaripia, pumzi ya pua yake ilifunua vilindi vya bahari na misingi ya dunia ikaonekana.