2 Samuel 23:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, mashujaa watatu kati ya wakuu thelathini waliteremka wakati wa mavuno wakamfikia Daudi kwenye pango huko Adulamu. Wakati huo jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Refaimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya wale mashujaa thelathini wakuu walimwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, mashujaa watatu kati ya wakuu thelathini waliteremka wakati wa mavuno wakamfikia Daudi kwenye pango huko Adulamu. Wakati huo jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Refaimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati ambapo kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi kufika Bonde la Refaimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, mashujaa watatu kati ya wakuu thelathini waliteremka wakati wa mavuno wakamfikia Daudi kwenye pango huko Adulamu. Wakati huo jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Refaimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, hawa wakuu watatu waliomo miongoni mwao wakuu wa 30 wakashuka siku za mavuno, wafike kwa Dawidi penye pango la Adulamu; navyo vikosi vya Wafilisti vilikuwa vimepiga makambi Bondeni kwa Majitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, mashujaa watatu kati ya wakubwa makumi tatu waliteremuka wakati wa mavuno, wakamufikia Daudi kwenye pango kule Adulamu. Wakati ule kundi la waaskari wa Wafilistini lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Refaimu.