2 Samuel 23:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale mashujaa wake watatu walitoka, wakapenya katikati ya kambi ya jeshi la Wafilisti, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, karibu na lango la mji, wakamletea Daudi. Lakini Daudi alikataa kuyanywa, na badala yake, akayamwaga chini kama tambiko kwa Mwenyezi-Mungu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale mashujaa wake watatu walitoka, wakapenya katikati ya kambi ya jeshi la Wafilisti, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, karibu na lango la mji, wakamletea Daudi. Lakini Daudi alikataa kuyanywa, na badala yake, akayamwaga chini kama tambiko kwa Mwenyezi-Mungu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwenye kile kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu na kumletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa; badala yake, aliyamimina mbele za BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilichokuwa karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; lakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale mashujaa wake watatu walitoka, wakapenya katikati ya kambi ya jeshi la Wafilisti, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, karibu na lango la mji, wakamletea Daudi. Lakini Daudi alikataa kuyanywa, na badala yake, akayamwaga chini kama tambiko kwa Mwenyezi-Mungu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wale mafundi wa vita watatu walipojipenyeza makambini mwa Wafilisti, wakachota maji katika kisima cha Beti-Lehemu kilichoko langoni, wakayachukua, wakamletea Dawidi, lakini hakutaka kuyanywa, akammwagia Bwana kuwa kinywaji cha tambiko,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale mashujaa wake watatu walitoka, wakapenya katikati ya kambi ya kundi la waaskari wa Wafilistini, wakaenda na kuchota maji katika kisima cha Betelehemu, karibu na mulango wa muji, wakamuletea Daudi. Lakini Daudi alikataa kuyakunywa, na pahali pa kuyakunywa, akayamwanga chini kama vile sadaka kwa Yawe,