2 Samuel 23:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abishai nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa mashujaa thelathini. Yeye alipigana kwa mkuki wake dhidi ya watu 300, akawaua, akajipatia jina miongoni mwa wale mashujaa watatu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu mia tatu ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abishai nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa mashujaa thelathini. Yeye alipigana kwa mkuki wake dhidi ya watu 300, akawaua, akajipatia jina miongoni mwa wale mashujaa watatu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye aliyekuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abishai nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa mashujaa thelathini. Yeye alipigana kwa mkuki wake dhidi ya watu 300, akawaua, akajipatia jina miongoni mwa wale mashujaa watatu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Abisai, ndugu yake Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu miongoni mwa watu watatu; yeye ndiye aliyeuchezesha mkuki wake juu ya watu 300; ndio, aliowaua, akawa mwenye macheo kwa hao watatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abisayi mwana wa Zeruya na ndugu ya Yoabu alikuwa mukubwa wa mashujaa makumi tatu. Yeye alipigana kwa mukuki wake na watu mia tatu, akawaua, akajipatia sifa pamoja na wale mashujaa watatu.