2 Samuel 23:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Benaya mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa theluji, alishuka shimoni na kuua simba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Benaya mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa theluji, alishuka shimoni na kuua simba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabzeeli, ambaye alifanya mambo mengi ya ushujaa. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni siku kulipokuwa na barafu na kumwuua simba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wawili wakali wa Moabu, pia aliingia katika shimo na kumwua simba wakati wa theluji;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Benaya mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa theluji, alishuka shimoni na kuua simba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Benaya, mwana wa Yoyada, mwana wa mtu mwenye nguvu, alifanya matendo makuu, nako kwao kulikuwa Kabuseli. Yeye aliwaua wana wawili wa Arieli wa Moabu, tena siku moja, theluji ilipokuwa imeanguka, akashuka shimoni, akaua simba mlemle.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Benaya mwana wa Yehoyada wa muji Kabuseli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa teluji, alishuka katika shimo na kuua simba.