2 Samuel 23:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vilevile, aliliua jitu la Misri. Mmisri huyo alikuwa na mkuki, lakini Benaya alimwendea akiwa na fimbo tu, akamnyanganya mkuki huo, na kumwua Mmisri huyo kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vilevile, aliliua jitu la Misri. Mmisri huyo alikuwa na mkuki, lakini Benaya alimwendea akiwa na fimbo tu, akamnyang'anya mkuki huo, na kumwua Mmisri huyo kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia alimwua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumwua kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyang'anya Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vilevile, aliliua jitu la Misri. Mmisri huyo alikuwa na mkuki, lakini Benaya alimwendea akiwa na fimbo tu, akamnyanganya mkuki huo, na kumwua Mmisri huyo kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye ndiye aliyemwua mtu wa Misri aliyetisha kwa kutazamwa tu; namo mkononi mwake huyu Mmisri alishika mkuki. Lakini akamshukia na kushika fimbo tu, akampokonya yule Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa huo mkuki wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, aliua mutu mumoja jitu wa Misri. Mumisri yule alikuwa na mukuki, lakini Benaya alimwendea akiwa na fimbo tu, akamunyanganya mukuki ule, na kumwua Mumisri yule kwa mukuki wake mwenyewe.