2 Samuel 23:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yafuatayo ni majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi: Yosheb-bashebethi, Mtakmoni, aliyekuwa kiongozi wa wale watatu, yeye alipigana kwa mkuki wake, akaua watu 800 wakati mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi: Yosheb-Bashebethi Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu mia nane, aliowaua katika pambano moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yafuatayo ni majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi: Yosheb-bashebethi, Mtakmoni, aliyekuwa kiongozi wa wale watatu, yeye alipigana kwa mkuki wake, akaua watu 800 wakati mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi: Yosheb-Bashebethi, Mtahkemoni, alikuwa ndiye kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua kwa siku moja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi: Yosheb-Bashebethi, Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua katika pambano moja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni, Hamkuu wa wakuu wa majeshi; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yafuatayo ni majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi: Yosheb-bashebethi, Mtakmoni, aliyekuwa kiongozi wa wale watatu, yeye alipigana kwa mkuki wake, akaua watu 800 wakati mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya ndiyo majina ya mafundi wa vita, Dawidi alio kuwa nao: Yosebu-Basebeti wa Takemoni, mkuu wa thelathini; yeye aliuchezesha mkuki wake juu ya watu 800; ndio, aliowaua kwa mara moja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haya ni majina ya mashujaa Daudi aliokuwa nao: Yosebu-Basebeti, wa muji wa Takemoni ndiye aliyekuwa kiongozi wa wale watatu. Yeye alipigana kwa mukuki wake, akaua watu mia nane mara moja katika vita.