2 Samuel 23:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu aliyefuata miongoni mwa wale mashujaa watatu alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, wa ukoo wa Mwahohi. Siku moja, Eleazari alikuwa pamoja na Daudi walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kupigana vita. Waisraeli waliwakimbia Wafilisti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai Mwahohi. Akiwa mmoja wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha Waisraeli wakarudi nyuma,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu aliyefuata miongoni mwa wale mashujaa watatu alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, wa ukoo wa Mwahohi. Siku moja, Eleazari alikuwa pamoja na Daudi walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kupigana vita. Waisraeli waliwakimbia Wafilisti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai, Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati walipowadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai, Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu aliyefuata miongoni mwa wale mashujaa watatu alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, wa ukoo wa Mwahohi. Siku moja, Eleazari alikuwa pamoja na Daudi walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kupigana vita. Waisraeli waliwakimbia Wafilisti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aliyemfuata ni Elazari, mwana wa Dodo, mwana wa mtu wa Ahohi; huyu alikuwa mmoja wao wale mafundi wa vita watatu waliokuwa na Dawidi, Wafilisti walipowatukana na kujipanga huko kupigana nao. Watu wa Waisiraeli walipokwenda zao mahali pa juu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu aliyefuata kati ya wale mashujaa watatu alikuwa Eleazari mwana wa Dodayi, wa ukoo wa Muahoa. Siku moja, Eleazari alikuwa pamoja na Daudi walipowatukana Wafilistini waliokuwa wamekusanyika kwa kupigana vita. Waisraeli waliwakimbia Wafilistini.