2 Samuel 24:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Daudi alisumbuliwa sana rohoni mwake baada ya kuwahesabu watu. Kwa hiyo, Daudi akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa tendo nililolifanya. Lakini sasa, ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi unisamehe mimi mtumishi wako, kwani nimefanya jambo la kipumbavu kabisa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambia Mwenyezi Mungu, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Ee Mwenyezi Mungu, sasa ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia Bwana, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee Bwana, nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Daudi alisumbuliwa sana rohoni mwake baada ya kuwahesabu watu. Kwa hiyo, Daudi akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa tendo nililolifanya. Lakini sasa, ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi unisamehe mimi mtumishi wako, kwani nimefanya jambo la kipumbavu kabisa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambia BWANA, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Ee BWANA, sasa nakuomba, uondolee mbali hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambia bwana, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Ee bwana, sasa ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia BWANA, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee BWANA, nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Daudi alisumbuliwa sana rohoni mwake baada ya kuwahesabu watu. Kwa hiyo, Daudi akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa tendo nililolifanya. Lakini sasa, ee Mwenyezi-Mungu, nakusihi unisamehe mimi mtumishi wako, kwani nimefanya jambo la kipumbavu kabisa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi alipokwisha kuwahesabu watu, moyo ukampiga; ndipo, Dawidi alipomwambia Bwana: Nimekosa sana kwa kulifanya hilo. Sasa Bwana, umwondolee mtumishi wako hizo manza, nilizozikora! Kwani nimefanya kisichopasa kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia BWANA, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee BWANA, nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Daudi alisumbuliwa sana katika roho yake kisha kuwahesabu watu. Kwa hiyo, Daudi akamwambia Yawe: “Nimetenda zambi kubwa kwa tendo nililolifanya. Lakini sasa, ee Yawe, ninakusihi unisamehe mimi mutumishi wako, maana nimefanya jambo la kipumbafu kabisa.”