2 Samuel 24:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wakati malaika aliponyosha mkono wake kuelekea mji wa Yerusalemu ili kuuangamiza, Mwenyezi-Mungu alibadilisha nia yake. Mwenyezi-Mungu akamwambia huyo malaika aliyetekeleza maangamizi kwa watu, “Basi! Yatosha; rudisha mkono wako.” Malaika wa Mwenyezi-Mungu alikuwa amesimama karibu na uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu, Mwenyezi Mungu akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Mwenyezi Mungu alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, Bwana akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa Bwana alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wakati malaika aliponyosha mkono wake kuelekea mji wa Yerusalemu ili kuuangamiza, Mwenyezi-Mungu alibadilisha nia yake. Mwenyezi-Mungu akamwambia huyo malaika aliyetekeleza maangamizi kwa watu, “Basi! Yatosha; rudisha mkono wako.” Malaika wa Mwenyezi-Mungu alikuwa amesimama karibu na uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu, BWANA alihuzunika kwa sababu ya maafa akamwambia malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna, Myebusi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu, bwana akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa bwana alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna, Myebusi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wakati malaika aliponyosha mkono wake kuelekea mji wa Yerusalemu ili kuuangamiza, Mwenyezi-Mungu alibadilisha nia yake. Mwenyezi-Mungu akamwambia huyo malaika aliyetekeleza maangamizi kwa watu, “Basi! Yatosha; rudisha mkono wako.” Malaika wa Mwenyezi-Mungu alikuwa amesimama karibu na uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna, Myebusi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Malaika alipoukunjua mkono wake kuuangamiza Yerusalemu, Bwana akageuza moyo kwa ajili ya huo ubaya, akamwambia yule malaika aliyewaangamiza watu: Sasa inatosha, ulegeze mkono wako! Naye yule malaika wa Bwana alikuwa penye kupuria ngano pa Myebusi Arauna.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wakati malaika aliponyoosha mukono wake kuelekea Yerusalema kwa kuuangamiza, Yawe alibadilisha nia yake. Yawe akamwambia yule malaika aliyetimiza maangamizi kwa watu: “Basi! Inatosha; rudisha mukono wako.” Malaika wa Yawe alikuwa amesimama karibu na kiwanja cha kupepetea ngano cha Arauna wa muji wa Yebusi.