2 Samuel 24:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa anawaua watu, alimwambia Mwenyezi-Mungu, “Tazama, Mimi ndiye niliye na hatia! Mimi mwenyewe nimekosa! Hawa watu wapole hawakufanya uovu. Nakusihi sana uniadhibu mimi na jamaa ya baba yangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambia Mwenyezi Mungu, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Mkono wako uwe juu yangu na nyumba yangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi, alipomwoma malaika aliyewapiga watu, akanena na Bwana, akasema, Tazama, ni mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya baba yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa anawaua watu, alimwambia Mwenyezi-Mungu, “Tazama, Mimi ndiye niliye na hatia! Mimi mwenyewe nimekosa! Hawa watu wapole hawakufanya uovu. Nakusihi sana uniadhibu mimi na jamaa ya baba yangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambia BWANA, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kufanya kosa. Hawa ni kama kondoo tu. Wamefanya nini? Mkono wako uwe juu yangu na nyumba yangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambia bwana, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Mkono wako uwe juu yangu na nyumba yangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi, alipomwona malaika aliyewapiga watu, akanena na BWANA, akasema, Tazama, ni mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya baba yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa anawaua watu, alimwambia Mwenyezi-Mungu, “Tazama, Mimi ndiye niliye na hatia! Mimi mwenyewe nimekosa! Hawa watu wapole hawakufanya uovu. Nakusihi sana uniadhibu mimi na jamaa ya baba yangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi alipomwona yule malaika, jinsi alivyowapiga watu, akamwambia Bwana kwamba: Tazama, mimi nimekosa, mimi nimekora manza; lakini hawa kondoo wamefanya nini? Kwa hiyo mkono wako na unipige mimi na mlango wa baba yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi, alipomwoma malaika aliyewapiga watu, akanena na BWANA, akasema, Tazama, ni mimi niliyekosa, ni mimi niliyepotoka; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya baba yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi alipomwona yule malaika aliyekuwa anawaua watu, alimwambia, Yawe: “Mimi ndiye ninayekuwa na kosa! Mimi mwenyewe nimekosa! Hawa watu wapole hawakufanya uovu. Ninakusihi sana uniazibu mimi na jamaa ya baba yangu.”