2 Samuel 24:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Arauna alipoangalia upande wa chini alimwona mfalme akimkaribia pamoja na watumishi wake, naye akatoka, akaenda na kumsujudia mfalme, akainama mpaka chini ardhini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Arauna alipotazama na kumwona mfalme na maafisa wake wakija kumwelekea, alitoka nje na kusujudu, uso wake ukagusa chini mbele ya mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo Arauna akatazama, akamwona mfalme na watumishi wake wakimjia; Arauna akatoka, akasujudu mbele ya mfalme kifulifuli hata nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Arauna alipoangalia upande wa chini alimwona mfalme akimkaribia pamoja na watumishi wake, naye akatoka, akaenda na kumsujudia mfalme, akainama mpaka chini ardhini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Arauna alipotazama na kuona mfalme na watu wake wanakuja kumwelekea, alitoka nje na kusujudu mbele ya mfalme kifudifudi, uso wake mpaka ardhini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Arauna alipotazama na kumwona mfalme na watu wake wakija kumwelekea, alitoka nje na kusujudu mbele ya mfalme kifudifudi, akiuinamisha uso wake ardhini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo Arauna akatazama, akamwona mfalme na watumishi wake wakimjia; Arauna akatoka, akasujudu mbele ya mfalme kifudifudi hadi chini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Arauna alipoangalia upande wa chini alimwona mfalme akimkaribia pamoja na watumishi wake, naye akatoka, akaenda na kumsujudia mfalme, akainama mpaka chini ardhini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Arauna alipochungulia akamwona mfalme na watumishi wake, wakipanda kuja kwake; ndipo, Arauna alipotoka, akamwangukia mfalme usoni pake hapo chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo Arauna akatazama, akamwona mfalme na watumishi wake wakimjia; Arauna akatoka, akasujudu mbele ya mfalme kifulifuli hata nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Arauna alipoangalia upande wa chini alimwona mufalme akimusogelea pamoja na watumishi wake, naye akatoka, akaenda na kuinama uso mpaka chini mbele ya mufalme.