2 Samuel 24:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Arauna akamwuliza mfalme, “Kwa nini bwana wangu mfalme amenijia mimi mtumishi wake?” Daudi akamjibu, “Nimekuja kununua uwanja wako wa kupuria nafaka ili nimjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu ili tauni iliyowakumba watu ikome.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Arauna akasema, “Mbona bwana wangu mfalme amekuja kwa mtumishi wake?” Daudi akajibu, “Nimekuja kununua sakafu yako ya kupuria, niweze kumjengea Mwenyezi Mungu madhabahu, ili tauni iliyo katika watu iondolewe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Arauna akasema, Bwana wangu mfalme amemjia mtumwa wake kwa kusudi gani? Naye Daudi akasema, Makusudi ninunue kwako kiwanja hiki, ili nimjengee Bwana madhabahu, ili kwamba tauni ipate kuzuiliwa katika watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Arauna akamwuliza mfalme, “Kwa nini bwana wangu mfalme amenijia mimi mtumishi wake?” Daudi akamjibu, “Nimekuja kununua uwanja wako wa kupuria nafaka ili nimjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu ili tauni iliyowakumba watu ikome.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Arauna akasema, “Mbona bwana wangu mfalme amekuja kwa mtumishi wake?” Daudi akajibu, “Kununua sakafu yako ya kupuria, ili niweze kumjengea BWANA madhabahu, ili tauni iliyo katika watu iondolewe.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Arauna akasema, “Mbona bwana wangu mfalme amekuja kwa mtumishi wake?” Daudi akajibu, “Kununua sakafu yako ya kupuria, ili niweze kumjengea bwana madhabahu, ili tauni iliyo katika watu iondolewe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Arauna akasema, Bwana wangu mfalme amemjia mtumishi wake kwa kusudi gani? Naye Daudi akasema, Nimekuja kununua kwako kiwanja hiki cha kupuria, ili nimjengee BWANA madhabahu, ili tauni ipate kuzuiliwa kwa watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Arauna akamwuliza mfalme, “Kwa nini bwana wangu mfalme amenijia mimi mtumishi wake?” Daudi akamjibu, “Nimekuja kununua uwanja wako wa kupuria nafaka ili nimjengee Mwenyezi-Mungu madhabahu ili tauni iliyowakumba watu ikome.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Arauna akauliza: Ni kwa sababu gani, bwana wangu mfalme akija kwa mtumishi wake? Dawidi akamwambia: Ninataka kununua kwako hapa pako pa kupuria ngano, nijenge pa kumtambikia Bwana, huku kuuawa kwa watu kukomeshwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Arauna akasema, Bwana wangu mfalme amemjia mtumwa wake kwa kusudi gani? Naye Daudi akasema, Makusudi ninunue kwako kiwanja hiki, ili nimjengee BWANA madhabahu, ili kwamba tauni ipate kuzuiliwa katika watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Arauna akamwuliza mufalme: “Kwa nini bwana wangu mufalme amenifikia mimi mutumishi wake?” Daudi akamujibu: “Nimekuja kununua kiwanja chako cha kupepetea ngano kusudi nimujengee Yawe mazabahu kusudi ugonjwa mukali uliowapata watu ukome.”