2 Samuel 24:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme, chukua chochote unachoona kinafaa na utolee sadaka. Mimi nawatoa fahali hawa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na vifaa hivi vya kupuria na nira za ng'ombe kuwa kuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme na achukue chochote kinachompendeza na akitoe sadaka. Hapa kuna maksai kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia kuna miti ya kupuria na nira za ng’ombe kwa ajili ya kuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Arauna akamwambia Daudi, Bwana wangu mfalme na akitwae, akatolee yaliyo mema machoni pake; tazama, ng'ombe hawa kwa sadaka ya kuteketezwa, tena vyombo vya kupuria, na vyombo vya ng'ombe, viko kwa kuni,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme, chukua chochote unachoona kinafaa na utolee sadaka. Mimi nawatoa fahali hawa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na vifaa hivi vya kupuria na nira za ng'ombe kuwa kuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme na achukue cho chote kinachompendeza na akitoe sadaka. Hapa kuna maksai kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia kuna miti ya kupuria na nira za ng'ombe kwa ajili ya kuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme na achukue chochote kinachompendeza na akitoe sadaka. Hapa kuna maksai kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia kuna miti ya kupuria na nira za ng’ombe kwa ajili ya kuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Arauna akamwambia Daudi, Bwana wangu mfalme na akitwae, akatolee yaliyo mema machoni pake; tazama, natoa ng'ombe hawa kwa sadaka ya kuteketezwa, tena vyombo vya kupuria, na vyombo vya ng'ombe, viko kwa kuni,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme, chukua chochote unachoona kinafaa na utolee sadaka. Mimi nawatoa fahali hawa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na vifaa hivi vya kupuria na nira za ng'ombe kuwa kuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Arauna akamwambia Dawidi: Bwana wangu mfalme na apachukue tu, atambike, kama yalivyo mema machoni pake. Tazama, nakupa hawa ng'ombe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, nayo haya magari na vyombo vya ng'ombe nakupa kuwa kuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Arauna akamwambia Daudi, Bwana wangu mfalme na akitwae, akatolee yaliyo mema machoni pake; tazama, ng’ombe hawa kwa sadaka ya kuteketezwa, tena vyombo vya kupuria, na vyombo vya ng’ombe, viko kwa kuni,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Arauna akamwambia Daudi: “Bwana wangu mufalme, utwae chochote unachoona kinafaa na utolee sadaka. Mimi ninawatoa ngombe dume hawa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na vifaa hivi vya kupepetea na nira za ngombe kuwa kuni.