2 Samuel 24:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kuteketezwa na za amani. Basi, Mwenyezi-Mungu akayakubali maombi kwa ajili ya nchi, na ile tauni iliyowakumba Waisraeli ikakoma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha Mwenyezi Mungu akajibu kwa ajili ya nchi, nayo tauni ikakoma katika Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi akamjengea Bwana madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi Bwana aliiridhia nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kuteketezwa na za amani. Basi, Mwenyezi-Mungu akayakubali maombi kwa ajili ya nchi, na ile tauni iliyowakumba Waisraeli ikakoma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha BWANA akajibu kwa ajili ya nchi, nayo tauni ikakoma katika Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Daudi akamjengea bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha bwana akajibu kwa ajili ya nchi, nayo tauni ikakoma katika Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi BWANA aliiridhia nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Daudi akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu mahali hapo na kumtolea sadaka za kuteketezwa na za amani. Basi, Mwenyezi-Mungu akayakubali maombi kwa ajili ya nchi, na ile tauni iliyowakumba Waisraeli ikakoma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akamjengea Bwana hapo mahali pa kumtambikia, akamtolea ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vipaji vya tambiko vya kumshukuru. Ndipo, Bwana aliposikia akiombwa kwa ajili ya nchi hiyo, nako kuuawa kwao Waisiraeli kukakomeshwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Basi BWANA aliiridhia nchi, na tauni ikazuiliwa katika Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Daudi akamujengea Yawe mazabahu pahali pale na kumutolea sadaka za kuteketezwa na za amani. Basi, Yawe akayakubali maombi kwa ajili ya inchi, na ule ugonjwa mukali uliowapata Waisraeli ikakoma.