2 Samuel 24:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yoabu akamwambia mfalme, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na awaongeze Waisraeli mara mia kuliko walivyo sasa, nawe bwana wangu mfalme upate kuona ongezeko hilo kwa macho yako mwenyewe. Lakini, kwa nini wewe bwana wangu mfalme unapendezwa na jambo hili?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Yoabu akamjibu mfalme, “Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na azidishe jeshi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yoabu akamwambia mfalme, Bwana, Mungu wako, na awaongeze watu, hesabu yao ikiwa yo yote, mara mia, tena macho ya bwana wangu mfalme na yawaone; ila kwa nini neno hili limempendeza bwana wangu mfalme?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yoabu akamwambia mfalme, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na awaongeze Waisraeli mara mia kuliko walivyo sasa, nawe bwana wangu mfalme upate kuona ongezeko hilo kwa macho yako mwenyewe. Lakini, kwa nini wewe bwana wangu mfalme unapendezwa na jambo hili?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yaobu akamjibu mfalme, “BWANA Mungu wako na azidishe vikosi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Yoabu akamjibu mfalme, “ bwana Mwenyezi Mungu wako na azidishe jeshi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yoabu akamwambia mfalme, BWANA, Mungu wako, na awaongeze watu, hesabu yao ikiwa yoyote, mara mia, tena macho ya bwana wangu mfalme na yawaone; ila kwa nini neno hili limempendeza bwana wangu mfalme?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yoabu akamwambia mfalme, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na awaongeze Waisraeli mara mia kuliko walivyo sasa, nawe bwana wangu mfalme upate kuona ongezeko hilo kwa macho yako mwenyewe. Lakini, kwa nini wewe bwana wangu mfalme unapendezwa na jambo hili?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yoabu akamwambia mfalme: Bwana Mungu wako na aendelee kuwaongeza watu vivyo hivyo mara mia, naye bwana wangu mfalme na ayaone kwa macho yake! Lakini neno hilo bwana wangu mfalme analitakia nini?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yoabu akamwambia mfalme, BWANA, Mungu wako, na awaongeze watu, hesabu yao ikiwa yo yote, mara mia, tena macho ya bwana wangu mfalme na yawaone; ila kwa nini neno hili limempendeza bwana wangu mfalme?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yoabu akamwambia mufalme: “Yawe, Mungu wako, awaongeze Waisraeli mara mia kuliko walivyokuwa sasa, nawe bwana wangu mufalme upate kuona ongezeko hilo kwa macho yako mwenyewe. Lakini, kwa nini wewe bwana wangu mufalme unapendezwa na jambo hili?”