2 Samuel 3:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Paltieli akaenda pamoja na mkewe huku analia njia nzima mpaka huko Bahurimu. Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani.” Naye akarudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, mumewe alienda pamoja naye, akilia nyuma ya mkewe njia yote hadi Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani!” Kwa hiyo akarudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo mumewe akafuatana naye, akiendelea na kulia, akamfuata mpaka Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia, Haya, rudi. Naye akarudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Paltieli akaenda pamoja na mkewe huku analia njia nzima mpaka huko Bahurimu. Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani.” Naye akarudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, mumewe alikwenda pamoja naye, akilia nyuma ya mkewe njia yote hadi Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani!” Kwa hiyo akarudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, mumewe alikwenda pamoja naye, akilia nyuma ya mkewe njia yote hadi Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani!” Kwa hiyo akarudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo mumewe akafuatana naye, huku akilia, akamfuata mpaka Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia, Haya, rudi. Naye akarudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Paltieli akaenda pamoja na mkewe huku analia njia nzima mpaka huko Bahurimu. Abneri akamwambia Paltieli, “Rudi nyumbani.” Naye akarudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo mumewe akaenda naye akimsindikiza na kulia machozi mpaka Bahurimu; ndipo, Abineri alipomwambia: Nenda, urudi! Naye akarudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo mumewe akafuatana naye, akiendelea na kulia, akamfuata mpaka Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia, Haya, rudi. Naye akarudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Paltieli akaenda pamoja na muke wake akiwa analia njia yote mpaka kule Bahurimu. Abeneri akamwambia Paltieli: “Rudia kwako.” Naye akarudi.