2 Samuel 3:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kwenye lango kana kwamba anataka kuzungumza naye kwa faragha. Hapo Yoabu akamkata Abneri tumboni kwa sababu Abneri alikuwa amemuua Asaheli ndugu yake, na Abneri akafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando ndani ya lango, kama vile kuzungumza naye faraghani. Ili kulipiza kisasi damu ya nduguye Asaheli, Yoabu akamchoma mkuki tumboni palepale, naye akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hata katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hata akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kwenye lango kana kwamba anataka kuzungumza naye kwa faragha. Hapo Yoabu akamkata Abneri tumboni kwa sababu Abneri alikuwa amemuua Asaheli ndugu yake, na Abneri akafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando ndani ya lango, kama vile kuzungumza naye faraghani. Pale pale kwa kulipiza kisasi damu ya nduguye Asaheli, Yoabu akamchoma mkuki tumboni, naye akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando ndani ya lango, kama vile kuzungumza naye faraghani. Ili kulipiza kisasi damu ya nduguye Asaheli, Yoabu akamchoma mkuki tumboni palepale, naye akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hadi katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hadi akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kwenye lango kana kwamba anataka kuzungumza naye kwa faragha. Hapo Yoabu akamkata Abneri tumboni kwa sababu Abneri alikuwa amemuua Asaheli ndugu yake, na Abneri akafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Abineri alipofika Heburoni tena, Yoabu akamchukua langoni katikati na kumpeleka kando, apate kusema naye kinjamanjama; huko akamchoma tumboni, afe kwa ajili ya damu ya ndugu yake Asaheli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hata katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hata akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Abeneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimupeleka pembeni kwenye mulango sawa vile anataka kuzungumuza naye kwa siri. Hapo Yoabu akamukata Abeneri katika tumbo kwa sababu Abeneri alikuwa amemwua ndugu yake Asaeli, na Abeneri akakufa.